2014-09-15 15:54:05

Papa: Ndoa ni upendo wa Kristo: dhamana ya wanandoa.


Jumapili, Baba Mtakatifu akiongoza Ibada kwa ajili ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba, akiwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, pia alifungisha ndoa jozi ishirini za wanandoa. Katika homilia yake alikumbusha kwamba, Familia kama ilivyokuwa kwa wana wa Israel walipokuwa jangwani chini ya uongozi wa Musa, walipambana na changamoto nyingi , ikiwemo uchovu, ugomvi, mitafaruko,mizozo n.k, kama Somo la kwanza lilivyo eleza katika Liturujia ya Neno. Jozi Ishirini za wanandoa, walioketi kuzunguka madhabahu, wengi wao walikuwa katika umri wa zaidi ya miaka hamsini wenye kuwa na uzoefu mbalimbali katika maisha ya kifamilia. Wenye umri mdogo katika kundi hilo, hawakuwa chini ya miaka thelathini.

Msisimko na furaha vilionekana dhahiri katika nyuso za wanaume na wanawake waliofungishwa ndoa na Papa, baadhi ya mabibi harusi walitokwa na machozi. Baba Mtakatifu Francisco aliuliza kila mmoja kwa kumtaja jina lake, ataoe jibu lake mwenyewe waziwazi juu ya maamuzi yake, na katika utambuzi wa hali halisi za raha na taabu za kufunga ndoa.

Homilia ya Papa ililenga zaidi katika uzoefu halisi wa shida na taabu za maisha kama ilivyokuwa kwa wana wa Israel ambako hufika wakati wa kuchoka na safari hii ya Kanisa katika jangwa la dunia ya leo, wanamotembea watu wa Mungu, wengi wao wakiwa ni wanafamilia.

Papa alieleza ni vigumu kutoa hesabu ya nguvu kamili ya ubinadamu uliomo katika familia,akitaja misaada ya pande zote, msaada wa elimu, mahusiano katika ukuaji wa pamoja na ukuaji wa watu, kushirikiana katika furaha na matatizo. Familia ni mahali pa kwanza, ambamo binadamu wote hupata majiundo yao ya kwanza katika ubinadamu na pia ni tofali la kwanza, katika ujenzi wa jamii. Lakini Papa alionya, maisha ya ndoa na familia ni mwendo unaopita katika njia ya jangwani, na ambayo huweza wakati mwingine huchokesha, na kupungukiwa na vitu hata msingi kama maji na chakula, ni njia yenye kujaa majaribu mengi yanayoshonikiza kurudi nyuma.
Papa alieleza kwa kuwafikiria watu wa ndoa wanaokosa uvumilivu, ambao wameshindwa kuchota maji kutoka kisima cha Sakramenti ya Ndoa. Ambao wanayaona maisha hayo kila siku inayopita kuwa safari nzito na ngumu, na wakati mwingine yenye kutia uchungu.

Papa alieleza na kuhoji katika hali hiyo, mtu afanye nini, kurudia maisha ya furaha? Papa anasema, kwa njia ya nyoka ya shaba iliyotolewa na Musa, Mungu anapeleka nguvu zake za uponyaji, kwa huruma yake nyenye nguvu zaidi kuliko sumu ya vishawishi vya shetani. Katika Injili Yesu, anatutaka sisi kusikia na kuitambua ishara hii ya Msalaba.Kuwa na imani kwa Yesu msulubiwa, huruma ya Mungu yenye kuponya sumu inayoua dhambi.

Dawa ambayo Mungu anatoa kwa watu, Mwanae pekee, kufa juu ya Msalaba, ambayo kila mwenye kuitumia dawa hiyo, hasa, bibi na bwana harusi, hawawezi tena kusimama katika njia ya kuumwa na nyoka wa ibirisi, mwenye kuleta majaribu ya kuvunjika moyo, ugomvi, uzinifu, kutelekezwa ... Kama una imani katika Yeye, huponya kwa upendo na huruma, kwa damu yake iliyotiririka kutoka Msalaba wake, kwa nguvu ya neema hiyo ambayo huchipusha upya raha na matumiani yote ya kutembea katika barabara ya ndoa na maisha ya familia.


"Upendo wa Yesu, ambao huweka wakfu muungano wa mume na mke, una uwezo wote wa kudumisha upendo wao na kumfanya mpya binadamu aliyepoteza hamu na matumaini katika njia yake ya maisha. Kwa Upendo wa Kristo furaha ya bibi na bwana harusi kutembea kwa pamoja hurejea upya diama ; kwa sababu, ndoa ni safari ya pamoja ya mwanaume na mwanamke,ambamo wana jukumu la kusidiana mmoja kwa mwingine bila kuchoka".


Papa aliendelea kusema kuwa, ni kawaida kwa wanandoa wakati mwingine kuwa na ugomvi. Lakini kila inapojitokeza hivyo, Papa alishauri ni vyema kuikamilisha siku kwa amani. Ni kuomba samahani na kuendelea kutembea pamoja. Papa aliwatakia wanandoa wote, hija njema ya maisha, safari ya neema na kukua katika upendo. "Kutakuwa na misalaba, lakini Bwana, siku zote, atatembea pamoja nasi na kutusaidia kusonga mbele. Bwana awabariki nyote", Papa alikamilisha homilia yake. .







All the contents on this site are copyrighted ©.