UNCTAD, chombo cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia masuala ya
biashara na maendeleo, ni chombo muhimu katika masuala yote ya biashara, masoko,
uwekezaji , mikopo, teknologia, wajasilimali na utoaji wa misaada ya maendeleo kwa
ujumla. Chombo hiki (UNCTAD) kiliundwa mwaka 1964 kwa lengo la kusaidia maendeleo
endelevu katika nchi zote zenye viwanda vichache duniani, nchi maskini.
Mikutano
yake mikuu inapofanyika ni huzungumzia masuala ya biashara kwa ujumla na kutafuta
muafaka pale inapojitokeza migogoro na utofauti wa maendeleo ya uchumi na pia kutokana
na mabadiliko ya siasa. 15 - 26 Septemba 2014, unatarajiwa kufanyika Mkutano
Mkuu wa Biashara na maendeleo huko Geneva Uswisi, sanjali na maadhimisho ya miaka
50 ya UNCTAD. Kardinali Peter Turkson Rais wa Baraza la Kipapa katika uzinduzi
wa Mkutano Mkuu wa UNCTAD, anatarajia kutoa mchango wa Kanisa Katoliki katika shirika
hili , kwa mujibu wa Mtaguso Mkuu wa pili wa Vatican .
Tangu mwanzo Baraza
hili limekuwa na wasiwasi kutokana na kuongezeka kwa matatizo ambayo hata leo,
sehemu kubwa ya watu wanazidi kuteseka. Mtaguso wa pili wa Vatican ulitaka chombo
chake kuchochea Jumuiya katoliki kukuza maendeleo katika maeneo yao na jamii katika
haki ya kimataifa. "Mtakubaliana kila mtu kwamba maendeleo hayo ni lazima kusaidiana
ili kuondokana na matatizo makubwa ya wanadamu, na maendeleo hayo yanapaswa kukuzwa".Ripoti
inasema. Miaka mitatu baada ya kuanzisha chombo, cha Umoja wa Mataifa UNCTAD 1964
kimejishughulisha na masuala ya maendeleo, hasa biashara ya kimataifa. Na Baraza
kuu la kipapa walifanya mkutano na Papa Paulo wa IV , ambaye alitambua upeo wa mbali
wa chombo hiki cha UNCTAD na kuona kuwa ni chombo bora kitakachoweza kufanya kazi
daima na hasa pale kilipotoa tamko kuhusu“Maendeleo na jina jipya la amani” Zaidi
ya miaka 50 baadae, teknolojia mpya imevunja hali ya utamaduni na jadi katika mipaka
ya mataifa na kufunguliwa kwa maeneo mapya na pia kukawepo fursa za kiuchumi. Aidha
nguvu za uchumi zimepotea, na hasa kutokana na mapinduzi ya viwanda inayozidi kukua
kwa haraka katika Asia ya Mashariki inayokwenda sambamba na mabadiliko ya utendaji
mzima wa mfumo wa biashara ya kimataifa. Lakini kuna swali la msingi ambalo bado
linabaki yaani ni aina gani ya biashara na maendeleo inayotazamiwa kukutana na changamoto
kama vile kuenea kwa umaskini na ukosefu wa usawa wa maendeleo? Papa Paulo wa
VI alifafanua ukweli na uwazi kamili wa maendeleo kwamba: “mendeleo ya kweli ni
lazima kumwendeleza kila mtu kwa maneno mengine kila mtu binafsi (mwanamme, mwanamke
na watoto)kila kundi la binadamu, na binadamu kwa ujumla . Kwa nyakati zetu lakini,
Papa Francis amesema kuwa"hadhi ya kila binadamu na kutekeleza azma ya manufaa ya
wote ni wasiwasi unaodai kuboreshwa kwa sera za uchumi wote, kuliko kujaza hotuba
za kisiasa katika mitazamo au mipango ya maendeleo “. Uongozi wa kibinadamu au
utawala bado unaonekana kuwa na mengi ya kujifunza kuhusu jinsi ya kuamuru masuala
ya uchumi kwa ustawi wa kila mtu na kwa ulinzi wa mazingira. Katika maneno ya
Papa Francis: "Kwa heshima kutokana na kujitosheleza na utamaduni wa kila taifa,
ni lazima kutokusahau kwamba dunia ni mali ya watu wote kwa maana ya watu wote; ukweli
tu kwamba baadhi ya watu wanazaliwa katika maeneo yenye rasilimali chache au wako
chini ya maendeleo,na hii haihalalishi wao kutothaminiwa au wakose heshima" Ripoti
ya Turkson inaeleza kwamba, dunia ni nzuri iwapo kuna utawala bora, umoja wa kimataifa,
na haja ya kutambua uwepo wa walio bado katika hali za umaskini,wanaohitaji kuinuliwa.
Mtakatifu Papa Yohane Paulo II alisema : umasikini siyo kama ni tatizo, lakini kama
kama haja ya kuinuka nak utembea pamoja katika kuijenga dunia ya haki na usawa kwa
kila binadamu kwa nyakti hizi na hata kwa siku za baadaye.
Anaongeza pia,
Dunia yetu inautajiri tele, shukrani kwanza kwa ukarimu wa Muumbaji. Biasahara hakika
ni ufunguo muhimu katika kuongoza maendeleo na itasaidia kukuza maendeleo halisi ya
binadamu.