2014-09-10 16:13:13

Ugonjwa wa ebola ni tishio kwa dunia


Katika harakati zinazoendelea ya kupambana na hatari ya ugonjwa wa Ebola , Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNMI), limekutana siku ya Jumatano 10Septemba kuzungumzia juu ya hali nchini Liberia.

Na mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia Bwana Karim Landgren, alisema kuwa ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu Liberiasi inabidi kuangalia tena, kwani sasa nguvu zote nchini humo zinaangazia mlipuko wa ugonjwa huo.
Amesema kuwa tatizo la ugonjwa huo linahatarisha na kuaathiri Liberia katika hali ya utulivu wa kisiasa na harakati za ujenzi wa amani kwasababu ya wingi wa vifo, matatizo ya kiucumi , kijamii na kiusalama.

Tatizo kubwa la ugonjwa huo ndiyo lilitawala sehemu kubwa ya mkutano mzima wa Baraza la usalama, ambalo pia linatarajiwa kuongelea juu ya kuongeza muda wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia (UNMIL) kwasababu ya kukaribia mwisho wake ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.

Nchini Kenya Rais wa Uhuru Kenyatta ameahidi kutoa mchango wa dola milioni moja kwa mataifa ya Afrika Magharibi, Sierra Leone, Guinea na Liberia hili kuzisaidia kupambana na janga la Ebola ambalo linazidi kuwa tishio la nchi hizo.
Rais Uhuru alisema kuwa mchango huo ni ishara ya umoja katika kuzisaidia nchi zilizoathirika na janga hilo kuweza kupambana nalo.

Inasadikika kwamba Kwa ujumla, tangu mwanzo wa mwezi wa Agosti, UNICEF imesafirisha karibia tani 402 za vifaa vya kujikinga na madawa katika nchi zilizoathirika na Ebola; pamoja na juhudu hizo za kusambazaji lakini bado kuna upungufu wa vifaa na shirika hilo kuzidiwa nguvu katika kuwasaidia waathiriwa.
TKatika harakati hizo za kupamabana na Ebola na nchini Tanzania wameanza kujizatiti katika kukabiliana na ugonjwa wa huo kwa kuandaa mazingira mazuri ya kukabiliana na ugonjwa ikiwa utaingia nchini.
Rais Jakaya Kikwete Rais ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania , Jumanne 9Septemba alitembelea jengo maalum lililotengwa katika hospitali ya wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam kupokea watu watakao hitajika kufanyiwa uchunguzi wa ugonjwa huo, alisema kuwa, meamua kutembelea katika maeneo hayo muhimu ili kujionea mwenyewe kile anachoambiwa na wataalamu na pia kusikia katika vyombo vya habari.
Vile vile Rais alitembelea katika uwanja wa ndege kuoona jinsi gani wageni wanavyokagulliwa na vifaa maalumu vya kudhibiti ebola mara wanapotua nchini.
MAREKANI: KUWEKA KIPAUMBELE CHA USALAMA WA KITAIFA, BARAK OBAMA
Rais wa Marekani Barack Obama alisema jumuiya ya kimataifa inahitaji kuchukua hatua kuhusu mgogoro wa ugonjwa wa Ebola.
Alikiambia kituo cha televisheni cha NBC cha nchini Marekani kwamba uwezo wa jeshi la Marekani unahitajika kuweka vituo vilivyotengwa pamoja na vifaa na kutoa usalama kwa wafanyakazi wa afya wa kimataifa. “Kama hatutafanya juhudi hizo hivi sasa na kusambaa kwa ugonjwa huu sio tu kwa bara la Afrika lakini hata sehemu nyingine za dunia kuna uwezekano wa virusi hivyo kugeuka geuka na inakuwa rahisi sana kuambukiza wengine”.
Na aliongeza kuwa, anaamini kwamba Marekani inahitajika kuweka mpangilio wa kukabiliana na mlipuko wa Ebola kama kipaumbele cha usalama wa kitaifa.
UNESCO: Kujua kusoma na kuandika kunaweza kuleta maendelo endelevu:
Ni tamko lililosemwa wakati wa kilele cha Siku ya Kimataifa ya kujua kusoma na kuandika kilichofanyanyika Jumatatu 8Septemba ya wiki hii.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova alisema kuwa watu wanaojua kusoma na kuandika wanawezeshwa kuchukua uamuzi unaofaa katika mambo ya kiuchumi, ustawi wa jamii au mazingira, akiongeza kwamba wanawake wanaojifunza kusoma wanachangia katika kuleta maendeleo endelevu.
Aidha, UNESCO ilisissitiza kuwa vita na mizozo vinachangia katika kuzuia watoto kwenda shuleni, takwimu zikionyesha kwamba asilimia 42 ya watoto wanaoishi kwenye nchi maskini zilizoathirika na mizozo hawaendi shuleni.
Kuhusu mizozo hata Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema kwamba, wakati wanafunzi duniani kote wameanza mhula mpya wa shule, jambo hilo halijawezekana kwa watoto milioni 30 waliopo kwenye maeneo mbali mbali ya mizozo duniani kote.
Josephine Bourne ambaye ni Mkuu wa Mradi wa Elimu kwa Watoto Duniani (UNICEF) alisema mizozo, majanga na mapigano huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini, Iraq na Ukraine kunawanyima watoto hao haki yao ya msingi ya elimu, na idadi hiyo ni sawa na nusu ya watoto wote duniani wasiohudhuria shule.
Alitoa mfano kwamba watoto wanashindwa kwenda shule kwa sababu shule zimekuwa maeneo yanayolengwa wakati wa mashambulizi hali watoto wengine wanalazimika kukimbia makwao na kuishi maisha ya ukimbizini; alitoa mfano mwingine wa nchi za Sierra Leone na Liberia,kwani janga la Ebola limefanya shule zifungwe hadi mwisho wa mwaka huu.
Bi. Bourne alisema iwapo watoto wataweza kuendelea na shule, itakuwa ni kiashiria kuwa maisha yamerejea hali ya kawaida na kuwawezesha kuondokana na woga na hivyo kuweza kujenga maisha yao ya baadaye.
UNICEF iliwaomba usaidizi zaidi kwenye mpango wake wa dharura wa elimu ambao kwa sasa umechangiwa kwa asilimia mbili tu ya kiwango kinachotakiwa na hivyo kuwa na upungufu wa dola Milioni 247.

TANZANIA: MTIHANI WA KUMALIZA YA ELIMU YA MSINGI
Wakati Jumatatu 8Septemba ilikuwa ni siku ya kimataifa ya kujua kusoma na kuandika, nchini Tanzania Jumatano 10Septemba Wanafunzii zaidi ya laki nane walitarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi .
Mtihani huo ulitarajiwa kufanyika katika lugha mbili ya kiswahili na kingereza na pia kuzingatia hali zote za watoto wakiwemo wale wasio ona na wale ambao kuona kwao ni hafifu.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi , Jenista Muhagama Jumanne 9Septemba katika mazungumzo na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam alisema maandalizi yote kwa ajili ya mtihani yalikuwa yameisha kamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa karatasi za mitihani, fomu maalum (OMR) za kujibia mitihani pamoja na nyaraka zote muhimu zinazohusu mtihani huo.
Alitoa wito kwa kamati za mitihani za mikoa na wilaya kuhakikisha taratibu zote za mitihani zinazingatiwa ipasavyo na kuwataka wasimamizi, walimu, wananchi na wanafunzi kutoshiriki katika vitendo vya udanganyifu na kwamba atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria Katika mtihahani huo unategemewa kufanyika kwa siku mbili.
NA WATANGAZAJI WENU KUTOKA IDHAA YA KISWAHILI YA RADIO VATIKAN INAWATAKIA UFANISI MWEMA WANAFUNZI WOTE.









All the contents on this site are copyrighted ©.