2014-09-10 08:46:36

Iraki ;baraza jipya la mawaziri latangazwa


Jumatatu 8Sept 2014 nchini Iraq, baraza jipya la mawaziri limetangazwa, hata hivyo hakuna Waziri wa ulinzi wala wa mambo ya ndani ya nchi aliyetangazwa mpaka sasa. Lakini waziri mkuu wa nchi hiyo amesema atafanya uteuzi wa mawaziri hao kwa muda wa wiki moja.
Naye Waziri wa mambo ya nje wa marekani john Kerry amelikaribisha baraza jipya la mawaziri lililotangazwa nchini Iraq, na kusema kuwa baraza hilo litaleta manufaa ya taifa hilo.
Akisisitizia msimamo wa Marekani, alisema kwamba serikali yake itashirikiana kwa karibu na serikali hiyo.
Waziri Mkuu Haidar al Abadi, amewaambia waandishi wa habari kuwa huenda serikali hiyo ikasababisha nchi yake kuondokana na makundi ya wapiganaji wanaotishia usalama wa taifa hilo, endapo kutakuwa na kuaminiana miongoni mwa wananchi.
Nafasi nyingine za mawaziri zimejazwa kwa mujibu wa makubaliano kati ya Washia walio wengi, Wasunni hali kadhalika na Wakurd walio wachache.
Wakati hayo yakijri watu 12 wameuawa na wengine zaidi ya thelathini wamejeruhiwa jumatatu wiki hii katika shambulio la bomu liliyotegwa ndani ya gari dhidi ya msafara wa kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika AMISOM kaskazini mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadiscio, viongozi wa somalia wamethibitisha.
Abdulkadir Sidi, mkuu wa mkoa wa Shabelle ya Chini amabako shambuli hilo lilitiokea alisema kuwa “ Gari iliyojazwa vilipuzi ilisukumwa ikielekezwa kwenye kifaru cha Kikosi cha wanajeshi wa AMISOM na raia 12 wa kawaida waliokua wakisafiri ndani ya basi wameuawa na wengine 27 wamejeruhiwa na, Wanajeshi wawili wa AMISOM wamejeruhiwa pia katika shambulio hilo.

Wasiwasi wa vita umetanda Ukraina
Bado mashambulizi mapya yanaendelea kutokea mwanzo mwa wiki hii karibu na mji wa mwambao wa Marioupol, mwashariki wa Ukraine,miliyo ya risasi na mizito naendelea na kupelekea makubaliano yakusitisha mapigano kuwa hatarini.

Kundi moja la raia wa Ukraine waliyojitoa muhanga kwa kupigania uhuru wa Ukraine wameshambuliwa kwa bomu jumapili mwishoni mwa juma liliyopita kwenye moja ya ngome yao katika mji wa Marioupol, huku milipuko ya mabomu ikiendelea kusikika usiku mzima wa jumapili.

Hali ya wasiwasi imeendelea kutanda nchini Ukraine, licha ya viongozi wa Urusi na Ukraine kusaini makubaliano ya kusitisha mapigano mashariki mwa Ukraine.

Wakati wa mazungumzo ya simu pamoja na kansela wa Ujerumani, Angela Markel, rais wa Ukraine Petro Porochenko amejizuia kusema kinachoendelea mashariki mwa Ukraine, huku akiendelea kupongeza juhudi za kusaini makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Urusi na Ukraine mjini Minsk.

Rais porochenko amekuwa na imani ya kutuma tume ya waangalizi wa jumuiya ya usalama na maendeleo barani Ulaya kwenye eneo kunakoshuhudiwa mapigano, huku akiwa na imani kwamba masharti ya kusitisha mapigano yatakua yametekelezwa kabla ya kuunza kwa mazungumzo kati ya pande zinazo husika katika machafuko hayo.

Viongozi wa waasi wa Ukraine wamependekeza kuongezwa kwa ibara ya kuutambua uhuru wa maeneo yanayothibitiwa na waasi kwenye makubailiano ya kusitisha mapigano yaliyosainiwa mjini Minsk.

Misri : Ushirikiano wa nchi za Kiarabu wakubaliana kushirikikiana kupambana na wababe wa jihad
Mawaziri wa mambo ya nje wa jumuiya ya nchi za kiarabu, jumapili Septemba 7 mwaka 2014 mjini Cairo, nchini Misri walikubaliana kuchukua hatua zinazohitajilka kukabiliana na waislamu wababe wanaozusha vita vya jihad, pamoja na kutoa ushirikiano wao katika juhudi za kimataifa, kikanda au kitaifa kwa kupambana na makundi ya kiislam yenye silaha.
Katika kikao hicho mawaziri hao wamekubaliana kusitisha misaada ya kijeshi hususani silaha na vifaa vingine vya jeshi pamoja na fedha kwa makundi ya kiislam yenye silaha nchini Iraq na Syria.
Azimio la jumuiya ya nchi za kiarabu ni kujilinda kwa mataifa wanachama wa jumuiya hiyo dhidi ya vitisho vya Dola la Kiislamu pamoja na makundi mengine ya kiislam ya kigaidi katika ulimwengu wa kiarabu.
Katibu wa jumuiya ya nchi za kiarabu, Nabil Al Arabi alisema “ Hatutokubali kuendelea kwa vitisho hivyo ya Dola la Kiislamu”, .
Kuongezeka kwa makundi ya wapiganaji wa kiislamu wenye msimamo mkali imekuwa ni tishio kwa mataifa wanachama wa jumuiya ya nchi za kiarabu, hadi kupelekea baadhi ya mataifa hayo kuvunja ushirikiano wao na makundi hayo.
Azimio la jumuiya ya nchi za kiarabu linatoa fursa kwa taifa lolote mwanachama wa jumuiya hiyo kutoa ushiriki wake kwa Marekani ambayo imekua ikitoa wito kwa mataifa kushirikiana kwa pamoja dhidi ya Dola la Kiislam.
Kenya: Magazvana watakiwa kuunga mkono wito wa kujiuzulu
Rais Uhuru Kenyatta amewataka magavana wa Muungano wa Jubilee wanaounga mkono wito wa Cord wa kuandaa kura ya maamuzi kujiuzulu mara moja na kuwania upya nyadhifa zao.
RAIS Uhuru Kenyatta amewataka magavana wa Muungano wa Jubilee wanaounga mkono wito wa Cord wa kuandaa kura ya maamuzi kujiuzulu mara moja na kuwania upya nyadhifa zao.
Alisema magavana hao wanakwenda kinyume na sera ya muungano tawala kuhusu ajenda ya maendeleo.
Akizungumza jumapili 7Sept katika Kaunti ya Kericho alipohudhuria ibada katika Immanuel Africa Gospel Church (AGC), alisema viongozi wa Jubilee ni sharti waungane kupinga shinikizo la kuandaa kura ya maamuzi.
Huku akihutubia umati wa watu mjini Kericho baada ya kutoka kanisani, Rais Kenyatta alisema hakuna mgawanyiko baina ya chama chake cha The National Alliance Party (TNA) na kile cha Naibu Rais William Ruto, United Republican party (URP).
Aliwalaumu magavana waasi wakiongozwa na mwenyekiti wa Baraza la Magavana na kiongozi wa Kaunti ya Bomet Isaac Ruto kuwa wanasaliti muungano tawala wa Jubilee.Aidha aliwataka magavana waasi kuwaambia Wakenya ukweli kuwa watatozwa ushuru zaidi endapo kiasi cha fedha zinazotolewa kwa serikali za kaunti kitaongezwa. Alisema kuwa serikali haina fedha zaidi za kupatia serikali za kaunti.
Alishangaa kwa nini wakuu hao wa kaunti wamekuwa wakitaka waongezewe fedha zaidi, hali wameshindwa kueleza namna walitumia fedha walizopokea kwenye kipindi cha fedha cha mwaka uliopita.
Rais alitetea serikali yake dhidi ya madai kuwa inajaribu kudhoofisha ugatuzi, huku akisema kuwa Jubilee imekuwa ikifanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa inatekeleza katiba mwaka mmoja tangu kutwaa hatamu za uongozi.
Tanzania:onyo kwa vyama vinavyo vyenye uchochezi
Katika Kamati za Bunge linaloendelea nchini Tanzania ,baadhi ya taarifa na mapendekezo ya tume mbalimbali zinazidi kuchangamsha Bunge hilo, kwani baadhi ya Kamati za Bunge Maalumu la Katiba zimependekeza kuwekwa kwa masharti ya kudhibiti vyama vya siasa ambavyo vitaendesha siasa za uchochezi na ubaguzi wa dini, jinsia au kuegemea eneo fulani tu katika upande wowote wa Jamhuri ya Muungano kufutiwa usajili wake.
Pendekezo hilo lilitolewa kwa nyakati tofauti na Kamati Namba nane na Namba kumi wakati zikiwasilisha taarifa za mijadala yake, bungeni mjini Dodoma Ijumaa 5Sept ya wiki iliyopita. Kamati Namba nane ilipendekeza kuandikwa upya ibara ya 197 (2)(a-d) ya Rasimu ya Katiba kwa kuongeza masharti hayo.
Akisoma mapendekezo hayo, mjumbe wa kamati hiyo, Lucas Malunde alisema kamati hiyo inapendekeza kufutwa kwa chama ambacho kinakubali au kupigania matumizi ya nguvu au uchochezi kama njia za kufikia malengo yake ya kisiasa.
Alisema sharti hilo litahusika kama ikibainika chama cha siasa kitaonekana kupigania au kukusudia kuendesha shughuli za kisiasa katika upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano.
“Katika ibara 197 (4) kamati imependekeza Bunge linaweza kutunga sheria inayoweka masharti sawa yatakayohakikisha vyama vya siasa kuzingatia mipaka na vigezo na masharti ya ibara hiyo,” alisema.








All the contents on this site are copyrighted ©.