Idadi ya washiriki katika sinodi maalum ya Maaskofu yatajwa
Katibu Mkuu wa Sekretariati ya Sinodi Maalum kwa ajili ya Familia ya Oktoba 2014 hapa
Vatican, Askofu Mkuu Bruno Forte , wa Jimbo Kuu la Chieti- Vasco, katika mahojiano
na Redio Vatican, ametaja idadi ya washiriki wa sinodi hiyo kuwa 253 . Miongoni mwao
kutakuwa na jozi 14 za wanandoa.
Askofu Mkuu Bruno, amefafanua neno “Sinodi”
kwamba maana yake ni "kutembea pamoja. Na hivyo wakati wa mkutano huo wa Sinodi,
watu kutoka bara tano za Kanisa zima la ulimwengu, watatembea pamoja wakikiekea Kiti
cha Petro, kwa ajili ya kutafakari pamoja, “changamoto za Kichungaji katika mazingira
ya uinjilishaji. Na kwamba wingi wa washiriki 253 katika Sinodi hii,unaweka rekodi
nyingi katika historia ya Sinodi za Vatican, baada ya ile ya 1969 na 1985, katika
mtiririko huo, unaohusiana na mikutano ya Maaskofu katika ushirikiano wao na matumizi
ya Mtaguso Mkuu wa II.
Na kwamba, Mababa wa Sinodi watakuwa 191, ikiwa ni
pamoja na wakuu wa idara ya 25 Curia na 114 Marais wa Mabaraza ya Maaskofu: 36 kutoka
Afrika, 24 kutoka Marekani, 18 kutoka Asia (China, kutakuwa na Askofu Mkuu wa Taipei,
Msgr. Shan-chuan), 32 kutoka Ulaya, ikiwa ni pamoja na Kardinali Angelo Bagnasco Italia,
na 4 kutoka Oceania.
Aidha kutakuwa na washiriki wengine 62, ikiwa ni pamoja
na 8 kutoka ushariki wa kidugu na kanisa la Kiotodosi, akiwemo Patriaki Hilarion,
Mwenyekiti wa Idara ya Uhusiano wa Nje wa Upatriaki wa Moscow..Na kutoka Makanisa
ya Mashariki kutakuwa na wajumbe 13, pia kutoka nchi zenye vita, kama vile Iraq na
Ukraine, wakiwakilishwa na Askofu Mkuu Louis Sako na kutoka Makanisa Katoliki ya
Kigiriki-Katoliki Shevchuk. Aidha 13 watakuwa wanandoa ambayo watakuwa sehemu ya
wasikilizaji 38, wenye haki ya kuongea lakini si kupigia kura maamuzi ya Sinodi; kuna
Washauri wawili na pia kuna kundi la watalaam 16 , watakao fanya kazi za kusaidia
Sekretariati ya Sinodi Maalum. Miongoni mwa wajumbe walioteuliwa na Papa, ni Padre
Antonio Spadaro, Mkurugenzi wa gazeti Jesuit "Civilta Catoliki".
Wakati wa
wiki mbili za kazi, washiriki wa Sinodi, watatafakari juu ya matokeo ya rasimu ya
kufanyia kazi iliyosambazwa mwezi Juni. Lengo, anasema Kardinari Lorenzo Baldisseri,
Katibu Mkuu wa Sinodi, ni kwa "kutoa pendekezo katika dunia ya leo uzuti na tunu za
madili ya familia , kama ilivyotangazwa na Yesu Kristo zenye kufuta hofu zote na kuinua
matumaini endelevu."
Kama ambavyo ilikwisha tangazwa awali katika Mkutano
wa Kawaida wa Sinodi ya Maaskofu, kazi za Sinodi hii maalum kwa ajili ya Familia,
zitafuata mbinu mpya, katika upendeleo wa kuwa na washiriki wengi zaidi wa Mababa
wa Sinodi. Anaelezea kadi. Baldisseri, "kufanya marekebisho ya sheria au pengine
kuweka kuwa na marekebisho halisi katika baadhi ya vipengere", Na kwamba hawatarajii
kuwa na waraka wa mwisho mwishoni wa Sinodi hii maalum, kwa kuwa hii ni tu hatua
ya kwanza ya safari, itakayokamilika mwaka 2015, Oktoba 04-25, wakati wa Mkutano
14 wa Sinodi ya kawaida juu ya mada "Yesu Kristo ataonyesha siri na wito wa familia.