Maaskofu wa Cape Verde kuanza hija yakitume Vatican Jumatatu.
Maaskofu Katoliki katika Nchi ya Visiwa vya Cape Verde, wanatazamia kuanza ziara yao
ya kitume hapa vatican ambayo hufanywa na Maaskofu kwa kawaida kila baada yamiaka
mitano, kuyatembelea Makao Makuu ya Kanisa na kukutana na Papa, kwa lengo la kutoa
taarifa na uzoefu wa kanisa katika kipindi hicho cha miaka mitano na matazamio ya
utendaji katika kipindi kinachofuatia, ikiwa pamoja na ushirikiano na mshakamano kati
ya Maaskofu na Papa katika kuliendeleza Kanisa la Kristo. Kanisa Katoliki katika
viiswa vya Cape Verde, halina Baraza lake la Maaskofu, na majimbo yake mawili yaliyoundwa
moja kunako mwaka 1533 Jimbo la Santiago di Capo Verde, linaongozwa na Askofu Arlindo
Gomes Furtado na Jimbo la Mindelo, liliundwa mwaka 2033 na linaongozwa na Askofu Ildo
Dos Santos Lopes Fortes. Majimbo hayo yako chini ya Baraza la Maaskofu Katoliki linalounganisha
Maaskofu wa Senegal, Mauritania, Capo verde na Guinea Bissau , na pia ni mwanachama
katika Baraza la Maaskofu wanaozungumza Kifaransa Afrika Magharibi (CERAO), na SECAM.
Idadi kubwa ya raia wa Visiwa vya Cape Verde, ambavyo viko karibu na Pwani ya
Senegal, wapatao milioni 1.5, ni Wakatoliki wanaofikia asimia 93 ya raia wote, kwa
mujibu wa takwimu za Kanisa za Mwaka 2011. Na iliwahi kutembelewa na Baba Mtakatifu
Yohane Paulo 11, terehe 25-27 Januari 1990, ambayo ilikuwa ni ziara yake ya kimataifa
ya 45.