Masista wa SOM, wanaendelea na Mkutano wao Mkuu wa 44
Mjini Loreto tangu tarehe 24 Agost hadi 14 Septemba 2014, Masista wa Huruma ya Wahudumu
Hospitalini(SOM), wanaendesha Mkutano wao Mkuu wa 44 juu ya mada: Huruma na shufaka
– Moyo wa Karama yetu.
Mkutano huu ulioanza na mafungo ya kiroho kwa muda
wa wiki moja, unahudhuriwa na wajumbe Masista 31 kutoka India, Ufilipino, Marekani,
Madagascar, Nigeria, Italia na Poland, na unafanyika katika Taasisi ya Mtakatifu Yosefu
ya Loreto ya hapa Italia, kwa ajili ya kuandaa mipango ya utekelezaji kwa shirika
katika kipindi kingine cha miaka sita ijayo, ikiwa pamoja na uchaguzi wa Mama Mkuu
Mpya wa shirika na wajumbe wawakilishi wa Shirika hilo. Shughuli za shirika hili hasa
zinazolenga katika uwanja wa afya zilianza, miaka 193 iliyopita. Wajumbe wa mkutano
unaoendelea wanatazamia kukutana na Papa Francisco hapo tarehe 17 Septemba, mjini
Vatican.
Shirika la SOM, ambako kwa wakati huu lina wanashirika Masista 400,
linaongozwa kwa wakati huu na Mama Mkuu Paola Iacovone, lilianzishwa hapa Roma na
Binti Mfalme Teresa Orsini Pamphili Land mwaka 1821, na kuwa Shirika la kwanza la
watawa wa kike kuhudumu hospitalini katika jiji la Roma.Na pia walikuwa ni Masista
wa kwanza kuhudumia Hospitali Kuu ya Mtakatifu Salvatore ambayo sasa ni inajulikana
kama Hospitali ya Mtakatifu Yohane wa Mateso. Karama ya masisita hawa ni kutoa msaada
kwa jamii ya leo inayokabiliwa na mateso ya mwili na kisaikolojia hasa kwa wagonjwa
wanaolazwa hospitalini.
Pia kati ya shughuli katika utume wao ni kutoa msaada
kwa chama cha watu wa kujitolewa katika masuala ya afya”La Cometa Onlus” kilichoanzishwa
mwaka 2003, kwa pamoja na kikundi cha Walei wanaojishughulisha na kazi za kukusanya
fedha nakukuza mipango ya uratibu kati ya masisita waliotawanyika pande mbalimbali
za dunia, ikiwemo mipango ya kupanga watoto tokeo maeneo ya mbali.
Na hivyo
karibuni kumezaliwa tawi jipya la chama kinachojulikana kama Teresa Orsini , lililoanzishwa
huko Gravina Puglia , aliko zaliwa mwanzishi wa Shirika la SOM, ambacho kinajishughulisha
pia na malezi ya kiroho kwa Wamama vijana.
Na pia inaelezwa kwamba, mchakato
unaotafuta kumtaja kuwa Mwenye Heri mwanzilishi wa SOM, katika historia ya shirika
hili tayari umeanza na pia wanaye Mwenye Heri Sisita Raffaella Cimatti, aliyetangazwa
kuwa Mwenye Heri na Na Mtakatifu Papa Yohane Paulo II.