Mtandao wa kimataifa kwa ajili ya elimu wazinduliwa Vatican
(Vatican Radio) Baba Mtakatifu Francisko, alikutana na Wakurugenzi wa Taasisi ya
Kimataifa kwa ajili ya mtandao wa elimu inayojulikana kwa jina "Scholars Accurents",
yenye Makao yake makuu huko Argentina, ambalo hulenga kuunganisha shule na mitandao
ya elimu kutoka tamaduni na imani mbalimbali. Taasisi hii ilikuwa ni kati ya waliofadhili
tukio la Mechi ya mpira kwa ajili ya amani, siku ya Jumatatu katika uwanja wa michezo
wa Olympic hapa Roma.
Baba Mtakatifu Alhamis akizunguza kwa njia ya Video,
alirudia kuwashukuru Wakurugenzi wa Taasisi hii ya Scholars Accurentes kwa mafanikio
yaliyokwisha patikana na aliwahimiza kuendelea na juhudi zao katika ujenzi wa mwingiliano
kati ya tamaduni mbalimbali za kidini na elimu, na hivyo kuwa kama daraja la maelewano
na udugu. Papa alitaja thamani ya ujenzi wa madaraja na kusikiliza, katika dunia
yenye kuwa na vita na ghasia kama zinazosikika, na kutoa wito wa kutowaacha watoto
peke yao.
Baba Mtakatifu pia alifanya mkutano wa video kupitia mtandao na
wanafunzi katika nchi mbalimbali juu za mabara 5: Salvador, Afrika Kusini, Ulaya Uturuki
(Istanbul), Israel, Australia, Cameroon. Papa pia alijibu maswali ya wanafunzi. Baba
Mtakatifu Francisco, amezidua jukwaa la kimataifa la Digital kwa ajili ya kuziunganisha
shule mbalimbali duniani ambamo teknolojia, sanaa na michezo vinaweza kutumiwa katika
kuhimiza utamaduni wa kukutana na mwingiliano wa tamaduni hasa vijana.
Baba
Mtakatifu Francisko anaamini kuwa ni muhimu kuhamasisha utamaduni wa kukutana. Na
hivyo jukwaaa hili limeandaliwa katika mtazamo wa uadilifu wa dini katika maisha ya
kila siku. Na kwamba , juhudi hizi za "Scholas Occurrentes, zinatoa mwaliko kwa wenye
taaluma mbalimbali, kama madaktari, polisi, walimu , na hata vijana wasiokuwa na ajira,
kukutana kwa njia hii ya digital, kwa ajili ya kukuza mawasiliano katika kupeana
ujumbe wa amani. Papa anaamini njia hii itaweza kuwaunganisha watoto na vijana wengi
kwa mfano katika uwnaja wa michezo sanaa ambazo ni njia kuu katika majiundo ya kuzingatia
tunu za heshima ya utu wa mtu.
Wakurugenzi wa juhudi hizi za Scholas duniani,
José Maria del Corra na Enrique Palmeyro, wakizungumza na wanahabari wanasema, juhudi
hizi walisema, zinavutia kwa sababu, zimezaliwa na mpango wa awali wa Papa akiwa bado
Askofu Mkuu wa Buenos Aires, alifanya majaribio ya kujenga mtandao wa shule katika
misingi ya teknolojia, michezo na sanaa, kuwa na mafanikio. Na Papa aliwaomba wanaoendesha
mpango huu huko Buenos Aires, kuendeleza mradi huu duniani kote. Tarehe 19 Machi,
kulifanyika mkutano na Papa mjini Vatican na hapa baada ya mchezo wa amani kati ya
madhehebu, kama ilivyokuwa imeandaliwa na “ Scholas Foundation na Argentina PUPI Onlus”.
Mkutano huo umefuatiwa na mkutano mwingine wa siku ya Jumatano wiki hii katika ukumbi
wa sinodi wa hapa Vatican. Na Alhamisi, Papa Francis wa Wajumbe wa taasisi hii, katika
ukumbi wa wa Sinodi, ambamo Papa alizungumza na kuweza kufuatiliwa na shule zilizo
katika mtandao huu katika bara tano.
Papa analenga hasa kutumia matukio ya
mechi za michezo, sanaa, na hasa teknolojia, kusaidia utamaduni wa mkutano na juu
ya matukio hayo badala ya kwenda vitani , na kumsaidia kijana kukua kama ndugu, lakini
bila ya kupoteza utambulisho wa utamaduni au dini yake. Ujumbe wa Papa unasema, "Kuna
vita ya kutisha yenye kuharibu ubinadamu: hii basi ni jaribio la kuleta pamoja vijana
na hata watu wazima katika kujenga pamoja utamaduni kukutana watu mbalimbali kwa amani".
Mtandao huu ni kwa nchi zote nchi tajiri na maskini, na jukwaa linalokwenda
katika nchi zote za dunia. Ni mpango ambayo inatoa uwezo wa kushiriki na kuungana
na wote bila ya ubaguzi wa kidini , kitaifa au kimbali. Ni jukwaa la kuwaunganisha
wote kwa amani.