(Vatican Radio) Katika Maadhimisho ya Kitaifa ya SIku ya Kazi Marekani, Askofu Mkuu
Thomas Wenski ametoa maelezo juu waraka wa Kanisa, ambao umetoa mchango wa mafundisho
ya kijamii ya Kanisa kuhusu heshima ya kazi. Maelezo yake yamelenga katika msisitizo
unaotolewa na Papa Francisco, mara nyingi katika hotuba zake kuhusu haki kwa kazi,
na hasa heshima katika utu wa mtu.
Marekani, kila tarehe mosi Septemba, huiadhimisha
kama Siku ya Kazi, ambayo kwa mara ya kwanza iliofanyika mwaka 1882. Tangu hapo,
husherehekewa vyama mbalimbali vya wafanyakazi, kwa ajili ya uimarishaji wa uwezo
wa uchumi kwa taifa la Marekani.
Askofu Mkuu Wenski wa Miami, Mwenyekiti wa
Tume ya Baraza la Maaskofu Marekani kwa ajili ya Haki na Maendeleo ya Binadamu,
ambayo pia hutoa mwanga juu ya hali halisi mbalimbali ya wafanyakazi Marekani, amezungumzia
ukosefu wa ajira na matumaini kwa mamilioni ya watu na matatizo yanayo hitajika
kupata ufumbuzi.
Askofu Mkuu Francisko, katika tafakari yake, kwa tukio hili
la mwaka huu, amewakumbuka Wataktifu Yohane XXII na Yohane Paulo 11 waliotangazwa
kuwa Wataktifu na Papa Francis mwaka huu. Amewataja wote wawili kwamba michango yao
ilikuwa mikubwa katika mafundisho ya kijamii ya Kanisa juu ya heshima ya kazi na
umuhimu wake katika ustawi wa binadamu. Amesema, Mtakatifu Yohane Paulo II, aliitaja
kazi kuwa kipengere muhimu katika suala zima la maisha ya kijamii" (Laborem Exercens,
No 3) na Mtakatifu Yohane XXIII, alisisitiza haki za wafanyakazi kwamba kila mfanyakazi
anapaswa kupata ujira wa haki(Pacem in Terris, No 20).
Aidha amerejea msisitizo
wa Papa Francsiko ambaye ameongeza katika maelezo ya watangulizi wake kwamba, kila
kazi lazima iandamane na heshima msingi ya utu mtu, sote tukiwa na hali sawa kama
watoto wa Mungu. Na alisisitiza umuhimu wake katika kudumisha umoja na mshikamano
si tu ndani ya familia lakini pia kijamii na katika ukuaji wa taifa moja.Kazi inatusaidia
kutambua ubinadamu wetu na ni muhimu kwa ustawi binadamu. Kazi si adhabu kwa ajili
ya dhambi lakini ni njia ambayo sisi, tunapaswa kuifanya kama zawadi kwetu wenyewe
na kwa kila mmoja na jamii zetu. Hakuna anayeweza kuendeleza ustawi wake au ustawi
wa jamii au taifa bila kazi na heshima na majitoleo ya nguvu katika mshikamano wa
watu wote.
Kwa hiyo Askofu Mkuu Wenski, amesema, adhimisho la Siku hii ya Kazi,
hutoa nafasi ya kuona jinsi kazi katika taifa la Marekani, inavyokwenda sambamba na
maadili ya kujivunia ya utamaduni ma mafundisho Katoliki. Mwaka huu, baadhi ya Wamarekani
wamepata ahueni iliyowapa mpumuo wa utulivu na usalama kwa uwepo wa msaada kama kinga
dhdi ya ugumu wa maisha. Na myumbo wa ukuaji wa uchumi, unaosababisha pia myumbo
katika upatikanaji wa ajira, unatoa himizo kwa taifa la Marekani kujenga ajira zinaonyesha
kwamba nchi inaweza hatimaye kuwa na uchumi ponyaji baada ya miaka ya mateso na
maumivu ya kimaisha. Askofu Mkuu Wenski, amesisitiza uelimishaji juu ya maana
na heshima kazi , hasa kwa vijana kwa ajili ya kuwajengea matumaini katika kuunda
familia zao zilizo bora na imara. Kazi na maisha ya familia huenda sambamba, katika
maana kwamba hutegemeana moja kwa jingine. Na hivyo kazi linakuwa ni sharti kwa ajili
ya uanzisha familia mpya, kwa kuwa familia inahitaji njia ya kujikimu,kwa njia ya
kazi" (Laborem Exercens, No. 10). Na ameshauri kufuata mwongozo wa Papa Franciko,
katika kukataa uchumi wa kutengana ila kazi iwe ni utamaduni halisi ya kukutana
na kuunda umoja na mshikamano .