2014-09-02 15:44:34

Mkutano wa mwaka wa majadiliano kati ya tamaduni: dunia mashakani


Mwingiliano wa tamaduni na dini katika majadiliano, ni mandhari ya mkutano wa Saba juu ya Mazungumzano Kati ya Dini, ambao huandaliwa na Baraza la Ulaya kila mwaka. Kwa mwaka huu mkutano huo umefanyika kwa siku mbili tarehe 1-2 Septemba Mjini Baku, Azerbaijan. Tukio limewakusanya pamoja, wawakilishi kutoka ndini mbalimbali Wakristo, Waislamu, Wayahudi, Wabuddhist na hata kutoka makundi yasiyo amani Mungu. Kwa Kanisa Katoliki, Mjumbe wake ni Pafre Jean-Marie Laurent Mazas kutoka Baraza la Kipapa kwa ajili ya Utamaduni.
Padre Jean Marie Laurent Mazas, akihojiwa na Redio Vatican, ameeleza lengo la mkutano huo kwamba zaidi ni kuangalia mwelekeo wa kidini katika mazungumzano ya tamaduni. Na ni dhahiri kwamba, hali ya sasa dunia ni ya wasiwasi sana, kama Papa Francisco alivyokwisha sema, tuko katika Vita Kuu ya Dunia ya Tatu. Na hivyo ni muhimu kuwa na mkutano kama huu, si tu kati ya viongozi wa dini, lakini pia kati ya wenye mamlaka katika Baraza la Umoja wa Ulaya.

Kwa nia hiyo madhumuni ya Kanisa katika mkutano huu, ni kuongeza kilio cha muumini kwa Mungu, ili kwamba watu wote wapate zawadi ya amani. Madhehebu yote ya Kikristo, huhubiri maudhui hayo, na huelimisha kwamba amani ni upendo. Na jambo ambalo daima au kama ni wimbo wao kwa wote wanaohusika na maamuzi yanayogusa maisha ya jamii ni kwamba mazungumzo kati ya dini, ni mazungumzo kati ya jamii kwa ajili ya kufanikisha maisha yenye mwingiliano wa tamaduni bila kuathiri dini wala utamaduni wa mwingine. Na pia ni kushirikishana mawazo katika hoja nani hasa anayehusika na maisha ya kijamii anayepaswa kuhakikisha uwepo wa kanuni na masharti kwa ajili ya mazungumzo: jibu sahihi ni jamii yenyewe, kukanusha tabia za kuonea wengine au kudharau wengine, kuondokana na ufahari wa kuona dini yangu ni bora kuliko ya yule, vivyo hivyo haki za waaamini. Huu ni mlango kwa ajili ya kuingia katika mazungumzo na mtu wa dini nyingine.








All the contents on this site are copyrighted ©.