Maandalizi ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya Familia
Katika kuelekea kilele cha mkutano wa maandalizi ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya
familia, Ijumaa iliyopita 23.08.2014, gazeti la Oservatore Romano lilitoa tafakari
juu ya maandalizi ya sinodi hiyo inayotarajiwa kufanyika, Oktoba 2014.
L'0sservatore
Romano limeandika kwamba katika maandalizi ya sinodi maalumu ya maaskofu kwa ajili
ya Familiaitakayofanyika kuanzia 5 hadi 19 Oct 2014 kuna haja ya kuangalia vipengere
muhimu vinavyotokana na desturi ya kanisa, ili sinodi isichambue tu yaliyotoka katika
Mabaraza ya Maaskofu Katoliki lakini uwe ni wakati wa kusikiliza hoja zote zilizotolewa
na watu wote wa familia ya Mungu, ambao wanaalikwa kushiriki na kuwasindikiza kwa
sala katika kazi itakayofanyika .
Na pia limefafanua maana ya Sinodi, ambalo
katika kigiriki, ni neno ambalo lilitumika katika Injili ya Mtakatifu Luka analipoelezea
juu ya safari ya Maria na Yosefu walipokuwa njiani kumtafuta Yesu akiwa na miaka kumi
na mbili na walimkuta katikati ya walimu na waandishi wa ekalu la Bwana , akitenda
kazi ya baba yake.Ni neno linalotufanya hata sisi tuweze kutafakari.
Kuhusu
tafakari ya kutafutwa kwa Yesu aliyekuwa amepotelea hekaluni, naye Papa Benedikto
wa kumi na sita katika barua yake ya kitume ya Utoto wa Yesu sura ya 141 anaandika
kuwa : Luka anatumia neno synodi, yaani Jumuiya ya safari, akiwa na maana kwamba
ni neno la kitaalamu kuwa na maana msafara. Kwa mantiki hii fikira zetu labda tunaweza
kusema ni ubahili wa familia takatifu, na pia inawezekana kutushangaza lakini kumbe
inatuonyesha maana nzuri ya kwamba katika familia takatifu , uhuru na utiii vilikuwa
ni vitu vinavyopatana, vinavyokwenda pamoja. Mtoto wa miaka kumi na mbili alikuwa
ameachwa huru achague , ni namna gani ya kutembea na marafiki zake anaolingana nao
wakati wakiwa njiani. Lakini jioni wazazi wake walikuwa wakimsubiri arudi kwao.
Tukiangalia
mada ya habari hii tunapata mambo mawili yanayojisuka yenyewe ikiwa na maana yake
kuu..yaani tunapofikiria sinodi inayotajiwa kwa maana ya : kutafuta uwepo wa Yesu,
ambaye kamwe hajaacha kanisa lake, bali ameungani nalo bila kutenganishwa , ni
kama familia yake kweli .Na pia Kanisa lifanya uhusiano na Yesu katika uhuru na utii
ili kuacha Roho Mtakatifu ndiye aweze kuelekeza ukweli wa mambo yote. (Joh 16,13).
Ili
kuweza kujua zaidi Yesu na ndani ya kanisa, ki ukweli inabidi kujipanga upya na kujiweka
katika hali ya usikivu wa neno lake, ambao kadili siku zinavyokwenda na kupitia desturi
za kanisa ya kikristo. Tangu enzi za zamani wakati kanisa lilijikuta linapaswa kuchukua
uamuzi juu ya matatizo mapya .
Yaliyokuwa yanajitokeza na amabayo hata Yesu
alikuwa hakugusia, Kanisa lilijikuta lina sababu ya kutafuta namna ya kufanya na hasa
kuweka mafundisho na maelekezo yenye kuwa na msimamo mmoja wa kutekeleza , ili kutatua
matatizo hayo mapya., Kwa namna hiyo ikafanyika kanuni na mwongozo ambao ukaweza
kutunza imani kwa Bwana wake katika madiliko ya nyakati na tamaduni. Kwanza ilifanyika
sinodi na baadaye mtaguso , hivi ni vIpengere viwili vilivyo fanyiwa kazi kwa umakini
na kuweza kupata majibu ya yanayo endana sawia na Maandishi Matakatifu.
Katika
harakati za maandalizi ya sinodi kwa ajili ya kutangaza kwa shauku kubwa na uzuri
wa Injili ya familia , ya kujibu matumaini yake na kutibu walio umia roho ni
muhimu kukumbuka kwa matumaini ni kitu gani kiliandikwa katika muhutasari wa maadalizi
ya sinodi kiitwacho hati ya kufanyia kazi "instrumentum laboris" ya kwamba: “Katika
haraka hii ya kanisa kuu la Petro anayejiweka kwa unyeyekevu ya kusikiliza Roho Mtakatifu,
akitafakari juu ya changamoto za kitume za leo”
Kwa hiyo hatuna budi kuungana
na Jumuiya katika safari , kwa sala , na kuwa na subira ambayo ndiyo inayo lisha
amani hili kuamsha upendo , ambao Yesu Kristo anaipelekea kanisa , na imani hiyo
ianaendelela kutunzwa kwa uhuru na utii , aliyojifunza kuitii familia takatifu ya
Nazareth, ambayo ni kama nyumba ya baba ya kuzaliwa , kwa hiyo hata sisi sote tunayo
nafasi huko pamoja na kuwa na maisha magumu.