2014-08-26 12:26:28

Josef Wesolowski hana tena hadhi ya Kidipolomasia Vatican


Mkurugenzi wa Ofisi ya Habari katika Jimbo la Papa , Padre Federico Lombardi, SJ, siku ya Jumatatu alithibitisha kuwa, Mjumbe wa Kitume wa zamani, Josef Wesolowski, ni kweli amekata rufaa dhidi ya hukumu ya kumvuliwa hadhi ya Kidiplomasia na kuwa mtu wa kawaida mlei. Vatican imemvua hadhi ya kidiplomasia kutokana na tuhuma zilizotolewa dhidi yake kuhusu unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto, akiwa mwakilishi wa Papa katika Jamhuri ya Dominika, tuhuma zilizo tolewa Agosti mwaka jana. . Na kwamba rufaa yake itasikilizwa na kutolea maamuzi wiki chache zijazo, pengine mwezi Oktoba 2014.

Padre Lombardi alifafanua mbele ya waandishi wa habari kwamba, mwakilishi huyo wa zamani wa Jimbo la Papa, katika kisiwa cha Jamhuri ya Dominika, alivuliwa cheo hicho mara baada ya tuhuma kutolewa dhidi yake , na hukumu kutolewa mapema mwaka huu kwa mujibu wa sheria za Kanisa. Na mara baada ya mchakato wa rufaa yake kukamilika, Wesolowski anaweza kupambana na mashtaka ya makosa ya jinai katika mfumo wa mahakama za kawaida.


Padre Lombardi aliendelea kuweka bayana kwamba , ni muhimu kutambua kwamba, Nuncio wa zamani Wesolowski kwa sasa hahusiki na kazi zozote za kidiplomasia kwa Jimbo Takatifu, na hiyo ina maana kuwa hana tena kinga ya kidiplomasia, aliyokuwa nayo awali. Na utaratibu wa idara ya mahakama ya Vatican katika kezi kama hii , itaendelea kusikilizwa mara uchunguzi utakapokamilika na hukumu itatolewa kisheria. Padre Lombardi alieleza hili akirejea maelezo potofu ambayo yamekuwa yakitolewa katika baadhi ya vyombo vya habari, siku chache zilizopita. Alionyesha mshangao juu ya upotoshwaji huo, akisema, ni muhimu kutambua kwamba, tangu mwanzo wa kesi, mamlaka ya vatican, ilitoa maelezo sahihi juu ya jambo hili, tena bila kuchelewa katika mwanga wa ukweli kwamba Nuncio wa zamani Wesolowski, kwa tuhuma zilizotolewa dhidi yake, Vatican imemvua kuwa mwakilishi wa kidiplomasia wa Jimbo Takatifu.


Na hiyo ndiyo maana alirudishwa Roma mara moja. Hatua hiyo inaelezea jinsi Jimbo la Papa lilivyojali na kushirikiana na mamlaka katika Jamhuri ya Dominika kushughulikia kashfa. Jimbo la Papa halikuwa na chochote cha kufichaficha katika kesi hii, bali linaishughulikia kikamilifu kwa mujibu wa sheria za Vatican , na Papa Francisko yuko makini, akitaka haki itendeke bila kupendelea upande wowote.
Na hivyo Padre Federico Lombardi alimalizia kwa kuthibitishia tena waandishi wa habari kwamba, Nuncio wa zamani Josef Wesolowski tangu atuhumiwe, Jimbo la Papa lilimvua hadhi zote za kidiplomasia na kinga yake, na hivyo anaweza pia kushitatakiwa katika taratibu za mahakama za kawaida za kiraia.

Taarifa zinasema , Josef Wesolowski anakabiliwa na mashtaka pengine si tu katika Jamhuri ya Dominika, lakini pia katika taifa lake la kuzaliwa Poland.








All the contents on this site are copyrighted ©.