Hivi karibuni Mons. Josef Ballong wa Redio Vatican, alitoa tafakari juu ya kumbukumbu
ya hati ya kuzuia utumwa duniani. Kumbukumbu inayo fanyika kila tarehe 23.08 ya kila
mwaka ambayo ni siku ya kimataifa ya kukumbuka ukomeshaji wa watumwa inayo andaliwa
na Shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO kwa ajili ya kumbukumbu ya kwanza ya ukomeshaji
wa utumwa kwa 1791 huko Santo Domingo. Ni Siku ambayo ni muhimu iliyopelekea kukomeshwa
kwa utumwa wa watu weusi.
Katika maelezo yake Padre Ballong alisema kwamba
ni siku inayowakilisha majadiliano ya moja kwa moja na kukumbuka kipindi kigumu
cha kuhuzunisha katika historia ya kiafrika , kama vile Mtakatifu Yohane Paulo
wa Pili aliwahi kusema kwamba , “ni ukweli haya yalikuwa ni mauaji ya kinyama ambayo
kamwe hayatasauhulika.
Lakini watu wa kusahau haswa ni jamii ya waafrika
wenyewe, kwasababu ya kutokuwa na mwanga mpana juu ya jamii yao na historia kamili
ya kipindi kile cha utumwa na kutokujua kuwa wahusika walikuwa ni waafrika wenyewe.
Aliendelea kueleza kuwa iwapo wanaongelea sana juu ya hati hiyo ya kuzuia na juu
ya utumwa wahusika kutoka Ulaya, Marekani, na visiwa vya Caribian , ni dhahili
kwamba mara chache wanasahau kuongelea hata matukio haya juu ya ng’ambo ya pili
ya sahara.
Pamoja na majadiliano mengi ya kimataifa juu ya tukio hili kama
lile la kipindi cha misafara ya utumwa inakuwa vigumu kutambua wahusika wa jamii
za kiarabu kwa kipindi cha kale , ya kwamba nao pia ndiyo walikuwa wa mwisho kufanya
hati hii na ukomeshaji wa utumwa. Afrika yenyewe inapaswa kufanya chini juu kwaajili
ya viongozi wake na kuwatia moyo vijana ambao ndiyo kizazi kijacho, na kuwahamasisha
katika masomo ya kina zaidi yanayolenga, pia kufanya utafiti wa matukio yanayo husu
Afrika yenyewe. Kwa namna hiyo umoja wa Afrika unaweza kuwa ndicho kitu cha msingi
, kwasababu ya kuhamasisha kizazi kipya ,hili waweze kupata mafunzo juu ya afrika
mpya wawe na utambuzi,na ujuzi wa kuweza kutatua matatizo yanayojitokeza kama vile
ubaguzi na ukosefu wa haki.
Tatizo kubwa linalojitokeza lakini ni kile kitendo
cha viongozi wa afrika kutojali, na hii ni kwasababu ya kuendelea kujionyesha
matukio mbalimbali ya bara hilo. Matukio hayo ni kama yale yaliyopita na ya kihistoria
, yaani ya utumwa, na hata ya sasa kama vile matatizo ya wahamiaji. Padre anaendelea
kutoa maoni yake kuwa hili kuweza kufanikisha jambo hili inahitajika viongozi wa afrika
wajihusishe zaidi , na kwa kufanya hivyo inawezekana kabisa kuwa na mwamko katika
jamii na hata kutatua matatizo yaliyo makubwa juu ya vijana wa kiafrika kwa ujumla.
Ukosefu wa utambuzi kwa ujumla , au ukosefu wa kumbukumbu ya kihistoria katika jamii
, inasababisaha mfululizo wa matukio makubwa yanaoneekana. Anatoa mfano kwamba
tazama ni kitu gani kinachojitokeza katika nchi za ulaya ambapo upotezaji wa mila
na desturi, ukristo, katika jamiii mbalimbali zimesababisha kukosa muelekeo juu
ya hali mpya inayojitokeza.
Anasema kuwa watu wengi wakimbizi kutoka bara
la afrika na mashariki ya mbali , inawaopesha jamii ya Ulaya , ambayo daima imekuwa
na upungufu wa uzalendo, kwasababu hiyo wanaogopa kukutanan na hali mpya hii ya uhamiaji.
Hii
ni kutokana na tabia ya siku nyingi, ambayo matokeo yake ni hasi juu ya matazamo
wa wahamiaji wa kizazi cha pili na hasa wale waliozaliwa ndani ya nchi za ulaya,
na kuelimishwa katika utamaduni wa kiulaya. Pia alielezea kwamba udhaifu unaojitokeza
katika utambuzi wa dini ya ukristo , umesababisha vijana wengi kutafuta matawi
mengine ya hitikadi kali ya kiislam , na kukutana na walimu waongo wa kiroho, na
ndipo matukio yamejitokeza ambayo yamepelekea vijana wa ulaya, kuchagua wawe mashahidi
wa Jihad , na hata kujiingiza katika vitendo vya kighahidi, kitu ambacho kinachojionyesha
katika dunia hii ambamo imejaa wahuaji,haswa kwa kile kinachojionyesha katika macho
yao yaani dunia iliyo kosa thamani yake.