2014-08-23 10:21:36

Papa Franciko azungumza kwa simu na familia ya James Martini aliyeuawa kikatili.


Baba Mtakatifu kwa moyo wa huruma na upendo kwa jirani, Alhamis iliyopita, alipiga simu na kuzungumza na familia ya Mwandishi wa habari wa Marekani, James Martin, aliyeuawa kikatili huko Syria, wiki hii.
Mkurugenzi wa Ofisi ya habari Vatican, Padre Lombardi, amethibitidha taarifa iliyotolewa kwamba, wakati familia ya marehemu ikiwa imegubikwa na majonzi mazito, Baba Mtakatifu Francisco aliwapigia simu na kuzumgumza nao na kuwafariji. Familia hii, ilipigwa na mshangao na kuguswa kwa namna ya kipekee na upendo wa Papa Francisko, kwa watu waliofadhaika. Papa aliwapigia simu nyakati za usiku wa saa mbili , muda mfupi baada ya chakula cha jioni. Papa alipenda kuonyesha mshikamano wake na familia hii, iliyo katika lindi la majonzi makali. Mama wa Marehemu ni Makatoliki.
Papa alianza kuzungumza na Mama na kisha na baba yake, familia. Wazazi wa Marehemu James Martin, wanaishi Richmond, New Hampshire, wakiwa wameguswa na upendo wa Papa, walitoa shukurani zao nyingi kwa ukarimu wake.

Marehemu James Martini Foley, ameuawa akiwa na umri wa miaka miaka 40. Ni Makatoliki aliyehitimu katika Chuo Kikuu cha Wajesuit cha Marquette University Wisconsin Marekani katika masuala ya uandishi. Akiwa Syria aliandika taarifa za harakati za vita na ujumbe wa kibinadamu na daima aliiomba familia yake imsindikize kwa sala, na hasa kusali Rozari, aliyoiamini kama waraka wake wa ukombozi. Kabla ya kutekwa nyara alifanya kazi zake nchini Libya na baadaye Syria ambako alitekwa 2012.

Mama Foley amesema, anaonea fahari ujasiri wa mwanae alio uonyesha hata wakati wa kuyatolea sadaka maisha yake kwa ajili ya kujali mateso ya watu wengine na kuzindua ombi la kidharura kwa ajili ya kuwaokoa mateka wengine. Chuo Kikuu cha Maarquette, kimepanga 26 Agosti, kutafanyika Ibada ya Misa kwa ajili ya kumwombea Marehemu. Mkurugenzi wa ofisi ya habari Vatican, Padre Lombardi, anasema ni wazi familia ya James inahitaji faraja za kiroho.








All the contents on this site are copyrighted ©.