2014-08-23 14:34:27

Mkristo ni mtu anayethubutu kutoa!


Kheri za Mlimani ni muhtasari mkuu wa mafundisho msingi yaliyotolewa na Yesu. Hii ni dira na mwongozo kwa Wakristo. Yesu aliwaachia wafuasi wake amri kuu ya mapendo kwa Mungu na jirani, mambo yanayopaswa kumwilishwa katika uhalisia wa maisha ya waamini kila kunapokucha!

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anasema kwamba, Kristo ni mtu anayethubutu kutoa kile alichokirimiwa na Mwenyezi Mungu. Maisha ya Kristo yanapaswa kusheheni matendo makuu ya ukarimu kwa jirani unaotekelezwa kwa si kwa kupiga matarumbeta, bali katika hali ya usiri, ili yaonekane na Mwenyezi Mungu ambaye yuko sirini.







All the contents on this site are copyrighted ©.