Maaskofu wa Afrika Kusini wahuzunishwa na madhulumu dhidi ya Wakristo Iraq
Baraza la Maaskofu Katoliki la Kusini mwa Afrika, ambalo huunganisha Maaskofu wa
Afrika Kusini, Botswana na Swaziland, limekemea vikali vurugu za maonevu na mauaji
katikaUkanda wa Gaza na kama ilivyo Iraq ambako Jumuiya za kikristo zimekuwa chambo
cha utesaji na mauaji na kufukuzwa kutoka nchi yao.
Taarifa ya Maaskofu iliyotolewa
na Askofu Mkuu wa Pretoria, Askofu Mkuu William Slattery OFM, inasema kuwa katika
mwezi huu,ambamo Dunia inakumbuka kupita kwa miaka 100 tangu Vita ya Kwanza ya Dunia,
ilipoanzishwa, bahati mbaya hata kwa wakati huu , kuna matukio mengi ya kutisha yanayowafanana
na ilivyokuwa wakati huo wa vita ya kwanza ya dunia. Kwa maoni ya Maaskofu , inaonekana
kwamba, hakuna somo duniai iliyojifunza juu ya ubinadamu wakati wa vita hiyo ya kwanza
ya dunia. Kileo, hakuna tena vita , kimetokomea na hivyo mamilioni y awatu kuendelea
kuteseka na kuuawa bila huruma, Maaskofu wanasema.
Maaskofu wanataja pia
kwamba, sehemu mbalimbali za Afrika, kama ilivyo nchini Iraq na Syria na sasa katika
Gaza, zinakabiliwa na hali ya kutisha na kuogofya sana, yenye ushahidi wazi wa kufilisika
kwa maadili katika vita vinavyoendelea. Na katika asili yake, kwenye hali ambamo
kwa silaha zisizoweza kutambua kati ya wapiganaji na wasiokuwa wapiganaji, na ambapo
wenye mamalaka makubwa hufadhaishwa na mtindo wa kipekee wa watu kujitolea mhanga
kusheheneza miili yao wenyewe kwa mabomu makali bila woga, hivyo vita vya kisasa vinakuwa
na mweleko wa kutisha zaidi kuliko hata ilivyokuwa zamani.
Maaskofu kuwa kwa
hiyo, wanatoa ombi kwa serikali ya Israeli na Mamalaka ya Palestina kukomesha vita,
kusitisha vurugu na kuacha kuuana. Na pia wametoa wito kwa viongozi , kuwajibika wao
wenyewe kaiak kuehdhimu haki msingi za utu wa binadamu na haki za kutofautiana. .
Maaskofu wanasisitiza kwamba, amani inawezekana tu kwa kuketi pamoja katiak majadiliano,
na kufikia muafaka wa kujenga amani ya kudumu.
Na kwa Wakristo nchini Iraq,
Maaskofu wa Kusini mwa Afrika wanasema, ni unyama wa hali ya juu, kuw ana mawazo ya
kuwafukuza Wakristu nchini Iraki amba wamekuwa wakiishi ktika nchi hiyo tangu mwanzo
wa Ukristo, miaka zaidi ya elfu mbili iliyopita. Maaskofu wameonyesha kujali hali
ya mateso kwa Wakristo , na pia kwa ajili ya kuharibiwa kwa majengo ya makanisa ya
kihistoria, ambao ni urithi wa Wakristo wote si Wakristuìo wa Iraki tu, lakini dunia
yote. Wakitaja kile kinachoendelea Iraki ni uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Katika
tamko lao, Maaskofu wamewaambia watu wa imani zingine , wanaoteseka pamoja na Wakristo
kwamba, mioyo yao na maombi pia wako pamoja nao. Na kwamba, wanaheshimu mafundisho
mengi ya dini ya Kiislamu, na hasa huduma zao kwa maskini na wahitaji. Na hivyo wanatoa
wito kwa Waislamu aminifu ambao wanaamini katika ubinadamu wa kila mtu, wawasihi wale
wanaoendesha madhulumu dhidi ya watu wengine wasio waislam , wasitishe ukandamizaji
huu wa kutisha, na warejeshe amani kama mafundisho halisi ya dini ya Kiislamu yanavyosema.