Uvunjifu wa amani na utulivu ni hatari kwa ustawi na maendeleo ya watu!
Patriaki Bartolomeo wa kwanza wa Kanisa la Kiorthodox la Costantinopol katika tamko
lake anasema kwamba, hakuna dini wala imani yoyote ile inayoweza kuhalalisha nyanyaso
na madhulumu ya watu wasiokuwa na hatia. Kanisa halitakaa kimya na kuona watu wanadhulumiwa
na kuteswa; watu wakishindwa kuonesha uvumilivu wa kitamaduni na matokeo yake kusababisha
mauaji na mateso ya maelfu ya watu kwa misingi ya chuki za kidini na ubaguzi.
Patriaki
Bartolomeo wa kwanza anasema, wananchi wa Iraq kwa sasa wanakabiliwa na hali ngumu
ya maisha, kwani wengi wao wamelazimika kuyakimbia makazi yao bila hata ya kuchukua
mambo msingi katika maisha.
Patriaki Bartolomeo wa kwanza anapenda kuungana
na viongozi mbali mbali wa kidini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema, kuomba
msaada kwa ajili ya wananchi wa Iraq. Anawataka viongozi wa kidini na kiserikali kuanzisha
mchakato wa majadiliano yatakayosaidia upatikanaji wa amani ya kudumu nchini Iraq
NI
matumaini yake kwamba, Mwenyezi Mungu chemchemi ya amani na mapendo atawajalia waamini
wa dini mbali mbali kuishi kwa amani na utulivu na kwamba, misimamo mikali ya kiimani
haina tija wala mashiko!