2014-08-22 09:15:51

Tanzia: Kanisa laomboleza kifo cha Kardinali Edmund Szoka


Tunasikitika kutangaza kifo cha Kardinali Edmund Casimir Szoka, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Detroit Marekani, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 86, usiku w Jumatano 20 Augosti 2014, kama ilivyotangazwa na Jimbo Kuu la Detroit.

Alhamis Baba Mtakatifu Francisko mara alipo pata taarifa, alijiunga katika maombolezo ya msiba huu na kutuma salaam zake za rambirambi kwa njia ya telegramu kwa Askofu Mkuu Carlo Maria Vigano , Nunsio wa Marekani, akimwomba kufikisha ujumbe wake kwa Askofu Mkuu Allen H. Vigneron wa Jimbo Kuu la Detroit.
Katika salaam hizo Papa, amemtaja Marehemu Kardinali Szoka kwamba, alikuwa mtu mkalimu aliyefanya utume wake kwa majitoleo makubwa, miaka yake yote ya kulitumikia Kanisa. Kwa moyo wa maombolezo, Papa anamwombea mtumishi huyu wa Kristo na kanisa , huruma ya upendo wa Baba wa Mbinguni. Na pia kwa wale wote wanao omboleza kifo chake waweze kujazwa na tumaini la ufufuko wa Kristo. Na anawapatia baraka zake za kitume, faraja na amani katika Bwana.

Kardinali Szoka aliwahi kuwa Askofu Mkuu wa Detroit tangu 1981-1990, na aliendelea kusimamia serikali ya Vatican Nchi ya Vatican, wakati wa utawala wa Papa YohanaPaulo II na Papa Benedikto XVI.Kardinali Szoka alikuwa akiishi Nothville Marekani na alifariki Usiku wa Agosti 20 , katika hospitali ya Kudra ya Novi.
Taarifa fupi juu ya maisha yake inaeleza alistaafu kazi za kichungaji mwaka 2006, baada ya kulitumikia Kanisa kwa miaka sitini, kwa majitoleo thabiti ya bila kujihurumia, katika huduma ya ukuhani kwa Kristo na Kanisa lake.
Edmund Casimir Szoka alizaliwa Septemba 14, 1927, katika eneo la Grand Rapids katika familia ya Baba Casimir na Mkewe Mary Szoka. Baba yake alihamia Marekani kutokea taifa linaloitwa sasa Belarus na mama yake kutoka Poland.

Kardinali Szoka mwaka huu aliadhimisha miaka yake 60 ya Upadre, wasia uliopewa na Askofu Noa Juni 5, 1954, kutumikia Jimbo la Marquette. Aliteuliwa kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo Nybildat Gaylord Juni ya 1971. Baada ya kuliimarisha Jimbo la Gaylord, Papa Yohana Paulo II, alimteua kuwa Askofu Mkuu wa Detroit na kusimikwa Mei 1981. Na June 1988 aliteuliwa kuwa Kardinali na mfupi baadaye, kusimamia masuala ya uchumi katika Jiji la Vatican, mwezi Aprili mwaka wa 1990, akaacha kuwa Askofu Mkuu wa Detroit, na ofisi yake kurithiwa na Kardinali Adam J. Maida . Alifanywa kuwa Rais wa Utawala wa jiji la Vatican mwaka 1997, na rais wa Nchi ya Vatican City mwaka 2001.

Jimbo Kuu la Detroit, linasema punde litatangza utaratibu za mzishi yake.







All the contents on this site are copyrighted ©.