2014-08-21 14:56:14

Imetangazwa Mada ya Ujumbe wa Papa kwa Siku ya 48 ya kuombea amani Duniani (1 Januari 2015).



“Hakuna Mtwana, Wote ni Ndugu ”, ni Mada itakayoongoza Ujumbe wa Papa kwa ajili ya siku ya 48 ya Kuombea amani duniani, hapo Januari Mosi 2015. Hii ni mara ya pili kwa Papa Francisco kutoa Ujumbe wake kwa ajili ya siku hii , tangu alipochaguliwa kuliongoza Kanisa la ulimwengu, March 2013.

Baraza la Kipapa kwa ajili ya haki na amani , linaeleza kwamba, katika ujumbe wa mwaka ujao, Papa Francisko, anakumbusha kwamba, wengi wanafikri, utumwa ni jambo la zamani lililopitwa na wakati . Lakini kumbe, maovu haya bado yako, tena kwa nguvu katika dunia ya leo.

Mwaka jana Papa katika Ujumbe wake kwa tukio hili la Januari Mosi 2014, ulilenga zaidi katika baraka za udugu: kwamba, “Uduna Mungu mwenyewe kwa sura na mfano wake Mungu, na hivyo wote wana hadhi sawa. Lakini kwa bahati mbaya, kuna wachache wanaoiua hadhi hiyo, na hivyo kuvuruga hata amani yao. Papa alieleza amani, katika ukweli, hupatikana kwa kutambua ubindamu wa mtu mwingine kwamba ana hadhi sawa. Lakini nyakati hizi zetu, haki hii hufinyangwa na mambo mengi ya kuchukiza, yenye nyuso za kuwaingiza wengine katika utumwa mambo leo. Mfano kusafirisha wengine na kuwaingiza katika utendaji ulio kinyume na hadhi yao, mfano ukahaba, kazi ya sulubu, ungandamizwaji na matendo mengine ya kitumwa yanayo dharirisha hadi ya utu wa mtu hasa kwa wanawake na watoto. Hali hizi za kitumwa huonekana katika mambo mengi ya aibu, yanayofanywa na watu binafsi au vikundi,kwa ajili ya kujipatia faida au utajiri wa harakaharaka, ikiwemo kuzusha migogoro ya kisiasa, kama inavyosikika sehemu nyingi za dunia, na pia kipeo cha uchumi kinacho shamirishwa na uovu wa rushwa.

Ujumbe wa Papa unakumbusha utumwa ni jeraha la kutisha linalo taka kujifunua kwa wazi katika mwili wa jamii ya kisasa, na ni jeraha kubwa katika mwili wa Kristo! Ili kukabiliana na hali hiyo kwa ufanisi zaidi , zaidi ya yote kunahiajika kutambua kulinda hadhi ya kila mtu, na pia kuzingatia thamani yake katika udugu wa binadamu, kama hitaji msingi la kushinda vishawishi vya ukosefu wa usawa, unaosababisha mtu mwingine mwingine kuwekwa katika hali za kitumwa, na matokeo yake yanahitaji uwepo wa njia ya ukombozi kwa watu wote.

Na hivyo Lengo liwe kujenga ustaarabu ulio simikwa juu ya hadhi ya sawa wa binadamu wote, bila ubaguzi. Kwa hili, pia inakuwa ni muhimu kuwa na mabadiliko mapya katika kazi zote za malezi, elimu na utamaduni kwa ajili ya jamii, yenye kuongoza katika uhuru na haki na hivyo katika amani kwa watu wote.


Siku ya Dunia ya kuombea Amani , ilianzishwa na Papa Paulo VI, na husherehekewa kila mwaka tarehe Mosi Januari. Ujumbe wa Papa kwa ajili ya siku hii, hutumwa kwa Maaskofu wote duniani na pia kwa wajumbe wote wa Kidiplomasia wanaowakilisha Jimbo Takatifu , kama ujumbe wa kuanza mwaka mpya kiserikali.







All the contents on this site are copyrighted ©.