2014-08-19 10:06:55

Radio Bakhita yafungwa Sudan ya Kusini!


Serikali ya Sudan ya Kusini kutokana na kile inachodai kuwa ni sababu za usalama wa taifa, imeamua kuifungia Radio Bakhita inayomilikiwa na kuendeshwa na Jimbo kuu la Juba, kutorusha matangazo yake. Baadhi ya wanafanyakazi katika kituo hiki wametiwa mbaroni.

Radio Bhakita ilifungwa tarehe 15 Agosti 2014 baada ya kutokea kinzani kati ya Serikali na Chama cha Upinzani. Vituo kadhaa ya Radio nchini Sudan ya Kusini, vimefungiwa au vimepata shinikizo kutoka katika vikosi vya ulinzi na usalama kiasi kwamba, kwa sasa au vimesitisha huduma kwa muda au vinasua sua katika utekelezaji wa dhamana yake.

Mkataba wa amani ili kusitisha vita na machafuko ya kijamii na kisiasa bado haujatekelezwa na pande zinazohusika. Umoja wa Mataifa unasema, kwa sasa inaonekana kwamba, biashara haramu ya silaha inazidi kupamba moto Sudan ya Kusini, hali ambayo itasababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao!







All the contents on this site are copyrighted ©.