Wasalesiani waadhimisha miaka mia mbili ya kuzaliwa Don Bosco
Jumatano ya tarehe 16 Agosti 1815, ikiwa siku baada ya Siku Kuu ya Bikira Maria Kupalizwa
Mbinguni, iliendelea kuwa furaha kubwa kwa familia ya Francesco Bosco na Margherita,
kwa John Bosco kuzaliwa.
Kwa ajili ya maadhimisho ya kutimia miaka mia mbili
ya kuzaliwa kwa Don Bosco, mwanzilishi wa Shirika la Wasalesiani, Mkuu wa Shirika
la Wasalesiani, Padre Angelo Fernandez Artime, aliongoza Ibada ya Misa kwa ni hiyo,
katika kituo cha Kiroho cha Colle Don Bosco. Ibada iliyohudhuriwa na familia kubwa
ya wasalesiani wake kwa waume , akiwepo pia diwani wa eneo hilo. Don Artime,
katika mahubiri yake, alitaja furaha ya Wasalesiani kwa kuzaliwa kwa mwanzilishi
wa shirika lao, furaha ambayo huiishi muda wote, na iliyo huishwa zaidi wakati Don
Bosco , alipotangazwa Papa Yohana Paulo 11, kuwa ni Baba na Mwalimu wa Vijana, wakati
wa maadhimisho ya kutimia miaka mia tangu kifo chake kilipotokea. Padre Artime,
alirejea maneno ya Injili ya siku akisema, kwao unapaswa kuwa wimbo wa sifa na shukrani
kwa Mungu Mkuu, Baba mwenye huruma, kwa kulijalia Kanisa, Mtakatifu Yohana Bosco
kama rafiki, ndugu na baba wa vijana.
Homilia ya Padre Artime, iliendelea
kukitazama kipaji cha Don Bosco, na kubaini kwamba, ni majaliwa ya Mungu na zawadi
kwa Kanisa la ulimwengu, kwa kuwa kupitia kwake mikono ya mama Margaret, Don Bosco
aliweza kujenga njia ya urafiki na kuwa walimu mema wa maisha, hatua kwa hatua, na
kuchagiza moyo mkuu wa kuwa Mchungaji Mwema, akiyaiga maisha ya Yesu Mwalimu mwema,
katika maisha yake ya kila siku, na kuyaeneza mafundisho aliyoyapata toka kwa wazazi
wake na kanisa kwa vijana wengine.
Kwamba kijana, Bosco, ambaye ndani ya
moyo wake alikumbatia malezi ya Bwana wake kwa msaada wa Mama Mtakatifu Sana Bikia
Maria, alifanya kila linalo wezekana, ili kuhakikisha mapenzi ya Mungu yanatimizwa
kwa moyo wa furaha ya uchachi na heshima, na kukamilishwa kwa kuuangalia msalaba wa
Kristo. Na hivyo kuondoka nyumbani kwao, hakuonekani kama utukutu, bali neema ya Bwana
hadi alipompumua pumzi yake ya mwisho.
Don Bosco Don, kwa njia hii anakuwa
kioo, baba na mwalimu wa vijana, na katika kuiona ishara ya kudra ya Mungu kwamba,
ina msukumo wa kipekee kwa kila kusudi jema.
Padre Artime, alimalizia homilia
yake akisema, maadhimisho haya ya miaka mia mbili ya kuzaliwa Don Bosco, , inakuwa
ni nafasi ya kipekee na wakati huohuo ni changamoto inayodai maisha ya upendo kupitia
huduma ya elimu na huduma za kitume kwa wavulana na wasichana wa ulimwengu huu, kuwawezesha
kutambua kwamba maisha yao ni zawadi ya Mungu, kwa ajili yetu na ni tendo la Roho
Mtakatifu, katika kila mmoja wao , na katika kushirikishana ndoto zao, matarajio,
na matatizo. Vijana wakisaidiana kwa kushirikishana uzoefu, waelimishaji wa , wavulana
na wasichana, walio tayari kusimama kando ya wahitaji, katika safari ya maisha, kwa
sababu, kama Don Bosco, pia wanataka kuwa na furaha sasa na hata milele. Na hivyo
waanza mwaka wa Jubilee , kwa furaha kuu na kumtukuza Mungu kwa majaliwa ya kuzaliwa
Don Bosco.Na pia kwa ajili ya kugundua mahali ilipo furaha ya kweli inayozaliwa kutoka
katika kazi za nyingi na pengine nzito za kujituma , kama ilvyo kwa Mkulima kutoka
jasho wakati akiitumikia aridhi na baadaye huvuna matunda tele kwa furaha.