2014-08-18 10:13:39

Maisha ni safari ndefu inayofanywa kwa pamoja kama ndugu!


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu asubuhi, tarehe 18 Agosti 2014 kabla ya kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kuombea amani na upatanisho nchini Korea, amekutana na kuzungumza kwa ufupi na viongozi wa kidini kutoka Korea. Katika salam zake kwa viongozi hawa, Baba Mtakatifu amewashukuru kwa moyo wa ukarimu, upendo na udugu waliomwonesha kwa kumtembelea.

Anasema, maisha ni safari ndefu ambayo mtu hawezi kutembea peke yake. Kuna haja ya kutembea kwa pamoja kama ndugu mbele ya Mwenyezi Mungu. Huu ndio wito ambao Mwenyezi Mungu aliutoa kwa Ibrahamu, Baba wa Imani. Baba Mtakatifu Francisko anasema, wao wote ni ndugu, watambuane kuwa ni ndugu, ili waweze kutembea kwa pamoja.

Baada ya neno hili la shukrani, Baba Mtakatifu Francisko aliwapatia baraka zake za kitume na kuwaomba wao pia kumwombea katika maisha na utume wake.







All the contents on this site are copyrighted ©.