2014-08-18 15:05:58

Kanisa Lebanon laitaka Ulaya izuie madhulumu dhidi ya Wakristo Iraki


Mkuu wa Kanisa katika eneo la Antokia ya Siria , Mwenye Heri Yossef III, ametoa ombi kwa Ulaya izuie madhulumu yanayo endelezwa dhidi ya Wakristo Iraki.
Taarifa inasema, kile kinachoendelezwa dhdidi ya jamii ndogo ya Kikristo, katika eneo linalokaliwa na jamii kubwa ya Waislamu, eneo la nyanda za Ninawi, ni sawa na wimbi la tsunami, au ni janga la karne. Mwenye Heri Youssef III, Patriaki wa Antokia ya Shamu, ametoa kilio chake kupitia gazeti la Kifaransa "Ouest France", ambamo ametoa maelezo mapya na ombi la kidharura kwa nchi za Magharibi, kusitisha mauaji ya kikabila na kidini yanayo fanywa na wapiganaji wa Kiislamu, wanajihadi ISIS na kusaidia jamii ya Kikristo wa Iraq.

Patriaki wa Lebanon ametoa hoja hiyo, hasa kwa Umoja wa Ulaya, akiangalisha kwa taifa la Ufaransa, ambalo analitaja lina jukumu muhimu, na kama wajibu wake kusitisha ukiukwaji wa haki za binadamu na ubaguzi wa kutisha nchini Iraki. Anasema Ulaya inapaswa kupeleka ujumbe wake katika eneo hili la Mediterranean. Vinginevyo - anaonya - jamii ya Kikristo ya Iraq, Syria na Lebanon ambazo ni kati ya jumuiya kongwe za Mashariki ya Kati, inaweza kweli kutoweka pamoja na utamaduni na urithi wake wa milenia.

Pamoja na hilo, ameuomba umoja wa Ulaya, usitishe upelekaji wa silaha kwa mfululizo kwa makundi wanajihadi nchini Syria na Iraq, na pia kwa makundi kadhaa ya wastani wa upinzani katika Syria. Pia kuzingatia maamuzi yaliyofikiwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa , kuchukua hatua za haraka ili kusaidia kupunguza makali ya mazingira magumu zaidi kwa makundi ya watu wachache Iraq; ikiwemo uzingatiaji wa azimio la kisheria la Bodi, ili kuhakikisha kurudi mara moja kwa usalama wale wote walio lazimika kukimbia makazi yao na mali. Na pia ameomba kuongezwa kwa mara mbili zaidi misaada ya kibinadamu, ukiwemo msaada wa kidharura wa wakimbizi nchi jirani ya Syria.
Na Uswiss, Jumatano ya wiki hii Agosti 20, kutakuwa na mkesha wa kiekumeni wa maombi kwa ajili ya Wakristo wanaoteseka Iraki. Kama ilivyoandaliwa na Kanisa Katoliki, pamoja na wawakilishi wa Kiprotestanti, Orthodox, Waanglikana, wawakilishi wa jumuiya ya Yazidi, na mashirika mengi ya Waislamu na shughuli nyingine za ubinadamu kwa ajili ya Iraki.

Washiriki wote katika mkesha huu watapanda ua jeupe la rose, kama ishara ya amani na huruma kwa waathirika wa mateso. Mbele ya kukabiliwa na matukio ya kutisha, yanayosikika katika mikoa mbalimbali ya dunia, hasa katika kaskazini mwa Iraq - waandaaji wanasema, tunataka kuonyesha katika mkesha huu , mshikamano wetu kwa waathirika wote wa ukatili, mateso, uuaji hadi kulazimika, kukimbia kutoka nyumba zao na kutoka kwenye vijiji vyao ili kuokoa maisha yao.

Na wakati huohuo, Caritas Uswisi imeomba serikali ya shirikisho, kukubali uwezekanavyo wa kusaidia wakimbizi wa Iraki kwa wakati hii kama ilivyofanya wakati wa Kosovo, Uswiss ilitoa hifadhi kwa wakimbizi wengi. Na kwa ujasiri Caritas, imeonyesha matumaini ya kuanzisha tena uwezekano wa maombi ya kufungua jalada kwa ajili ya hifadhi katika balozi, ili kuokoa watu na kuwapa makazi, hasa wanaposafiri katika nchi hatarishi.










All the contents on this site are copyrighted ©.