2014-08-17 13:28:37

Vijana Asia wapania kuimarisha imani kwa Kristo


Baada ya Baraka ya Mwisho kuhitimisha maadhimisho ya Ibada ya Misa katika uwanja wa Haemi, Askofu wa Daejeon, Peter Kang U-il, alitoa maelezo mafupi kwa Papa Francisko, juu ya kweli kwamba, vijana Katoliki Asia, wakiwa wameshibishwa na imani moja katika Kristo, licha ya kutofautiana , hukusanyika pamoja na kuvunja kuta za utaifa, na lugha, wakithibitisha udugu wao katika Kristo, na kusifu na kumtukuza Mungu kwa pamoja. Na wanaendelea kumtukuza Mungu hata kwa ajili ya wakati huu, ambamo wameweza kwa muda wa siku kadhaa kuwa karibu na Papa, na hivyo kuongeza imani y ao ,uzoefu, wingi wa neema na kujichosia wapania kuimritea mbegu ya matumaini ya baadaye.

Baada ya salamu Askofu wa Daejeon, pia Rais wa Baraza la Mabaraza la Asia, Kardinali Gracias, pia alitoa neno, ambamo alieleza hisia za vijana 10,000, waliokamilisha mkutano wao wa siku 5 kwa maamuzi thabiti ya kuwa wafuasi wa habari njema kwa nguvu ya ubatizo, kutembea katika njia ya Kristo, katika maisha yao ya kiraia. Na hivyo , ni kusema hapana kwa uchumi wa kutengwa, hapana kwa uchumi wa ubinafsi, hapana kwa moyo wa ubinafsi, na hapana kwa roho ya kupenda vitu vya kimwili, ni hapana kwa yote yaliyo kinyume katika kuipata furaha ya kweli, na ndiyo kubwa katika kukutana binafsi na Yesu, ambaye wanataka kumbemba mioyo mwao siku zote. Ni ndiyo kwa kilio cha maskini, na wapweke na waliosahaulika pembezoni. Ni ndiyo kwa shauku kusubiri ujio wa Kristo. Kardinali Gratias, alikamilisha salaam zake kwa kutangaza kwamba, Siku ya Vijana Duniani ijayo ya mwaka 2017, itafanyika barani Asia nchini Indonesia.









All the contents on this site are copyrighted ©.