Hotuba ya shukurani kutoka kwa Kardinali Andrea Yeum Soo-jung
Baada ya Maadhimisho ya Ibada ya Misa Takatifu Kardinali Andrew Yeoum Soo Jung, alitoa
hotuba ya shukurani kwa Papa Francisko, ambaye ameonyesha upendo mkuu kwa taifa la
Korea. Alisema, Baba Mtakatifu, kwa niaba ya watu wote wa Korea, walei pamoja watawa
na viongozi wa dini wa kanisa zima la Korea, kwa mara ingine ninakukaribisha kwa
furaha kuu.
Kardinali alirejea historia kwa ufupi akisema, Kanisa Katoliki
Korea tayari lina watakatifu 103 na mashahidi wafia dini 124, kwa kuongeza ulio
watangazwa leo kuwa Wenye heri. Na kwamba, eneo hili kuzunguka Gwanghwamun, imekuwa
ni kitivo cha historia kutokana na wahenga waamini wengi, kuwa mashahidi wafia dini
wa imani Katoliki.
Kardinali aliendelea kueleza kwamba Kanisa Katoliki Korea,
kwa damu waamini mashahidi wafia dini iliyomwangika, imethibitisha kuwa mfano mzuri
wa kuigwa na jamii yote ya Korea katika kukuza unyofu wa moyo na haki za binadamu.
Na Hivyo, Kardinali alionyesha tumaini lake kwamba , maadhimisho ya Ibada ya kuwataja
wenye heri iliyokamilika limekuwa ni tukio linalo dai kujenga amani na umoja wa Wakatoliki
si tu Korea lakini Pia watu wa Korea na jamii yote ya watu wa Asia, kupitia utandawazi
wa udugu.
Kardinali alimhakikishia Papa kwamba, Kanisa la Korea siku zote,
hujitahidi kuwa mwanga na chumvi ya Uinjilishaji duniani na katika kuwa mhudumu
wa maskini, wateswa, waliotengwa, kwa kuwafariji kwa furaha ya Injili. Kardinali Soo-jung
alikamilisha hotuba yake kwa kuomba baraka za Papa kwa Kanisa nchini Korea.