2014-08-15 12:34:04

Makanisa Sierra Leone yatoa jibu kwa kipeo cha Ebola


Licha ya changamoto nyingi, zinazosababishwa na ukosefu wa vifaa na maandalizi ya kutoasha katika kukabiliana na mfumko wa virusi vya ebola, Makanisa nchini Sierra Leone, yameanzisha mipango ya kujenga utambuzi zaidi juu ya maradhi hayo hasa katika namna za kuzuia na kutoa msaada kafara wa ebola.

Ebun James DeKam,Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa Sierra Leone(CCSL) , anaripoti kwamba, kwa msaada unaotolewa na Muungano wa Makanisa, wameanzisha kampeni ya nguvu kwa makanisa , kwa ajili ya kuielimisha jamii, mbinu za kupambana na kipeo cha ebola.

Sierra Leone ni kati ya mataifa ya Afrika Magharibi, yaliyopatwa na mfumko mkubwa wa wagonjwa wa ebola, ambao kwa sasa umekuwa kitisho cha nguvu kwa maisha ya watu kimataifa, tangu ugonjwa huo ulipo gunduliwa mwaka 1976. Na tangu ufumke Afrika Magharibi umeaua zaidi ya watu elfu moja.

DeKam ameonyesha matumaini yake kwamba, kanisa lina uwezo mkubwa katika kushawishi watu, kukubali yanayotakiwa kufanyika katika kipindi hiki cha hatari cha mfumko wa ebola. Na kwamba kila siku , ofisi yake hupokea taarifa za kinachoendelea juu ya ugonjwa huu na kuisambaza taarifa hiyo kwa watu mahalia na wabia wao wa kimataifa.

Aidha anasema , wameshikamana pia na vyombo vingine vya kidini kama vituo Katoliki vya Misioni , Kanisa la Petecoste, na Taasisi za Kiislamu katika juhudi za kupambana na ebola. Aidha viongozi wa kidini wameunda nguvukazi ya kupambana na ebola (RLTFE), ambayo imeandaa vipindi maalum vya masomo kwa jumuiya mahalia . Na kwamba viongozi wote wa kidini wameombwa wakati wa mahubiri yao , pia wazungumzie maradhi haya hasa namna ya kujikinga .

Mpaka sasa ugonjwa wa ebola hauna tiba wala chanjo. Ni vurusi vya hatari venye kusababisha kifo kwa haraka, na ambukizo lake ni kuwa na mahusiano ya karibu na mgonjwa wa ebola. Dalili zake ni kama homa ya mafua, kuumwa na kichwa na homa kali, na ikiendelea mgonjwa hutokwa na damu kwa mfululizo. Inatajwa tangu virusi kumeingina mtu hadi dalili kujitokeza huchukua kati ya siku tatu hadi 21 kutegemea na afya ya mtu.








All the contents on this site are copyrighted ©.