2014-08-14 13:26:25

Zawadi ya Papa kwa Baraza la Maaskofu Katoliki wa Korea


Papa amelizawadia Baraza La Maaskofu Katoliki Korea, nakala ya sanamu sura ya Kristo, iliyochongwa kwa mawe ya marumaru na kunakshiwa na rangi ya dhahabu. Sanamu hiyo ni nakala ya sanamu halisi ya karne ya IX, ambayo imewekwa mahali panapotuza palio takatifu chini ya madhabahu Kuu ya Kanisa Kuu la Kipapa la Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Sanamu hiyo inamwonyesha Kristo Mbarikiwa na Mwalimu, akiwa amefungua kitabu cha Injili, ambako kuna maneno” Mimi ndiye njia ya kweli ya uzima, kila anayeniamini mimi ataishi”.

Nakala ya sanamu aliyopewa Papa Francisko ina ukubwa wa cm 60 x 40,imetengenezwa kwa mfumo huohuo wa kijadi wa sanamu za mawe(”mosaic).








All the contents on this site are copyrighted ©.