2014-08-14 12:13:10

Vita kati ya Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini imeacha madonda makubwa ya utengano!


Rais Park Guenhye wa Korea ya Kusini, amemkaribisha Baba Mtakatifu Francisko nchini Korea kwa mikono miwili na kwamba, akiwa nchini humo atapata nafasi ya kutembelea maeneo kadhaa yenye utajiri mkubwa wa historia na maisha ya wananchi wa Korea.

Maeneo yote haya yatabakiza kumbu kumbu ya kudumu katika maisha na utume wa Baba Mtakatifu Francisko kwani Korea ya Kusini inakuwa ni nchi ya kwanza kutembelewa na Baba Mtakatifu katika Bara la Asia.

Rais Park kwa masikitiko makubwa katika hotuba yake amegusia vita na kinzani kati ya Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini. Hii ni vita ambayo imeacha madonda makubwa katika historia na maisha ya wananchi wa Korea kwa kuvuruga na kubomoa umoja na mshikamano wa kitaifa. Ni kinzani ambazo pia zimeleta utengano mkubwa katika maisha ya ndoa na familia, kwani familia nyingi zimesambaratika.







All the contents on this site are copyrighted ©.