2014-08-13 16:17:21

Papa Francisko, yuko njiani kuelekea Korea ya Kusini!


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano jioni tarehe 13 Agosti 2014 ameondoka mjini Vatican kuelekea nchini Korea ya Kusini kwa ajili ya hija yake ya kitume nchini humo, ambako anashiriki katika maadhimisho ya Siku ya Sita ya Vijana Barani Asia, inayoongozwa na kauli mbiu "Ondoka, uangaze, kwa kuwa nuru yako imekuja, na utukufu wa Bwana umekuzukia."

Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Fumicino, mjini Roma, Baba Mtakatifu amepata fursa ya kuzungumza kwa muda mfupi na Waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi pamoja na viongozi kadhaa wa Serikali na Kanisa, waliomtakia kheri na baraka tele katika hija yake ya kitume nchini Korea ya Kusini. Baba Mtakatifu Francisko kama kawaida yake, alijibebea mkoba wake na kupanda ndege, tayari kuanza hija hii ya kichungaji yenye matumaini makubwa kwa Kanisa Barani Asia.







All the contents on this site are copyrighted ©.