2014-08-13 09:42:29

Kumbu kumbu ya mauaji ya watu 560 huko Stazzema!


Baba Mtakatifu Francisko amemwandikia ujumbe Askofu mkuu Giovanni Paolo Benotto wa Jimbo kuu la Pisa, Kaskazini mwa Italia, katika kumbu kumbu ya miaka sabini, tangu watu 560, kati yao wakiwemo Mapadre wawili walipouwawa, huko Stazzema, Toscana na Vikosi vya Kinazi, tarehe 12 Agosti 1944.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe huu ambao umeandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican anamwomba, Yesu Mfalme wa amani, awawezeshe Watu wa Mataifa kujikita katika amani na utulivu. Anaendelea kuwakumbuka na kuwaombea watu wote walioathirika kutokana na mashambulizi haya. Anawaweka wote chini ya ulinzi na faraja kutoka kwa Bikira Maria.







All the contents on this site are copyrighted ©.