2014-08-08 11:46:07

Wakristu daima hubaki katika giza nene la mashambulizi ya Boko Haramu


Mashambulizi mapya Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, yanayo fanywa na Waislamu wenye msimamo mkali wa kikundi cha Kiislamu Boko Haram, ni jinamizi lenye kitisho kikali kwa wakazi wa eneo. Hivi karibuni watu wengi wasiokuwa na hatia wameuawa katika mji wa Gwoza na watu wengi wengi kulazimika kukimbilia kwa Cameroon. Aidha katika wiki za karibuni, mashambulizi mapya juu ya jamii ya Kikristo, kama yale yaliyofanyika Jumapili, Julai 27,katika shambulio la msichana kujilipua mwenyewe katika Parokia ya Mtakatifu Charles mjini Kano, na kuua watu wanne, ni mambo ya kuogofya sana.

Kardinali John Onaijekan, Askofu Mkuu wa Abuja, akizungumza katika mahojiano na Radio Vatican , juu ya dhuluma hizi hizi amesema, mashambulizi iwe yale yanayofanywa na moja kwa moja na Boko Haram, au yale ya kujitolea mhanga, au yale ya kuweka mabomu katika magari kulipuka, pamoja lakini lile la msichana kujiua baada ya kukaa na bomu ndani ya nguo zake kwa muda mrefu, ni jambo lililoshtua watu wote wenye mapenzi mema na hivyo limewatia jamii wasiwasi, jinsi mtu anavyoweza kukwepa uhalifu huu.


Na kwamba kwa ujumla, kwa wakati huu Wakristo, hasa katika eneo la Kaskazini , wanaishi kwa hali ya woga na mashaka makubwa. Na wanatambua wazi kwamba, makanisa ni malengwa na hivyo daima sasa wanajitahidi kwa kadri wanavyoweza kujilinda, lakini hawawezi kuwa na uhakika wa usalama wao mia kwa mia. Kwa mfano, hakuweza kufikiria kwamba msichana anakuja kanisani, anaweza kuwa amevalia mabomu na kujipua mhanga. Na hili limekuwa ni fundisho la kuchukua hatua mpya, cha kumchunguza kwa makini kila anayepita katika lango la Kanisa kuu, ingawa ni usumbufu. Kardinali anasema Wakristo wa Nigeria ni sehemu muhimu ya jamii ya taifa la Nigeria. Bahati mbaya sasa wanateseka mashambulizi haya, ambayo si tu kwa Wakristo lakini pia kwa watu wengine ikichukuliwa kwamba mashambulizi pia hufanywa pia katika masoko, taasisi za serikali na maeneo mengine ya umma na binafsi.


Akizungumzia juhudi serikali ya Nigeria kukabiliana na maasi haya anasema , ingawa serikali hutangaza kushinda vita dhidi ya Boko Haram, lakini matokeo yake hayaonekani hivyo, kwa sababu Boko Haram wanaendelea kushambulia na kuwa kitisho katika jamii. Baada ya karibu mwaka wa utawala wa kidharura, inashangaa, bado upinzani unaendelea na machafuko na kuleta majanga. Ni lazima kuwa na uhakika kwamba serikali ni kweli inatenda kwa nguvu, lakini kwa bahati mbaya inaonekana kuwa na wasiwasi mwingi katika ngazi ya kisiasa, na hasa ikizingatiwa kwamba mwaka ujao ni mwaka wa uchaguzi. Katika magazeti habari ya Boko Haram ni tu mistari michache katika gazeti; habari ya ukurasa wa kwanza, daima ni ni habari za kisiasa, zinazowahusu wakubwa. Matukio ya mashambulizi yanayofanywa na boko haram hupewa nafasi kidogo sana.









All the contents on this site are copyrighted ©.