2014-08-08 09:36:31

Ujumbe wa Papa kwa chama cha Knights of Columbus


Baba Mtakatifu Francisco amepeleka ujumbe kwa chama cha Kimataifa cha Knights of Columbus , kwa ajili ya Mkutano wake wa mwaka wa 132, uliofanyika huko Orlando Florida, tangu tarehe 5 -7 Agosti 2014. Katika Ujumbe huo uliotiwa sahihi na Katibu wa Vatican Kardinali Parolin, Papa ametoa wito kwa udugu wa jamii ya Knights ya Columbus, wawe chachu ya umoja kwa familia ya binadamu.

Mkutano huo uliongozwa na Mada “Nyote mtakuwa Ndugu : Miito yetu katika Udugu ni katika kuwa karibu na Moyo wa Baba Mtakatifu”. Mandhari hiyo iliyochaguliwa mwaka huu ni Wito unaodumu katika chama hicho tangu asili yake, kilipoanzishwa mwishoni mwa karne ya kumi na tisa.

Baba Mtakatifu katika ujumbe wake anasema, Imani inatufundisha kwamba, Kanisa limeitwa kuwa jamii moja, kaka na dada, watu wenye kusikilizana, kukubaliana na kutunza heshima ya kila mmoja na kutumika kama chachu ya maridhiano na umoja kwa familia nzima ya binadamu. Uaminifu wa Knights ya Columbus na maadili ya imani, ushirika na huduma, amesema, ina, si tu kuhakikisha kuendelea kwa uhai wa chama, lakini pia imechangia na inaendelea kuchangia utume wa Kanisa katika ngazi zote na, hasa, na huduma zima ya Kiti Kitakatifu cha Kitume.


Barua imethibitisha na kukiri juhudi za ushiriki wa kazi za Knights, katika kukabiliana na hali pinzani dhidi ya kanisa, hasa shinikizo la kutaka kuigandamiza dini katika mazingira ya umma, ili iwe tu kama ni jambo binafsi sana la mtu. Knights wamekuwa mstari wa mbele katika kutetea wajibu wa dini katika mazingira ya umma na kuhimiza ushiriki waamini walei katika kazi kijamii ili waweze kuonyesha ukweli wa Kristo. Papa Francisco ameeleza na kuirejea barua yake “ Kitume Injili ya Furaha” Evangelii Gaudium ambamo anasema, dunia ni nyumba ya kawaida ya kwetu sote , na sisi wote ni kaka na dada na kwa hivyo, hakuna mtu anayeweza kudai kuwa na haki ya kugandamiza ukuu wa dini kwamba ni jambo la urafiki wa kisiri siri kwa kundi la watu tu wasiokuwa na uhuru wa kuwashawishi wengine juu ya majiundo ya maisha ya kijamii na ya kitaifa, au kujali uhai wa taasisi za kiraia za kijamii, na bila uhuru wa kutoa maoni juu ya matukio yanayoathiri wananchi.


Baba Mtakatifu anasema , kama jinsi imani inavyopata sura yake katika matendo ya hisani, ambayo kazi zake huzaa matunda mazuri ndivyo, chama hiki kilichoanzishwa na Padre Michael MCGIVNEY na wanachama wa kwanza wa Knights ya Columbus, sura yake inaendelea kuonekana kwa matunda yake mazuri yanayotokana na shughuli zake mbalimbali za hisani, kupitia matawi yake ya mitaani, ambako huweza kukidhi mahitaji ya watu binafsi wahitaji na pia katika ujenzi wa jumuiya yenye imani katika umoja na mshikamano kwa manufaa ya watu wote. Ufahamu katika majitoleo ya sadaka ambayo humwaga upendo mkuu wa Kristo na Utakatifu wake kwa wengine, unaendelea kuwa moyo wa ujasiri Knights , katika kuteka msukumo mpya kutoka mafundisho na mfano wa Kristo ili kufikia wengine, hasa maskini na wanyonge, pamoja na uelewa wa dhati. Kama huduma ni roho ya udugu wenye kujenga amani (Ujumbe wa mwaka 2014 siku ya Amani, 10 World), basi kila kazi ya hisani inayofanywa na Chama cha Knights, inapaswa kutoa mwangwi wa upendo wa Kristo, na kutenda kazi katika ushirika wa mwili wake, yaani kanisa. Kwa kukaa ndani ya upendo, tunaona kwamba , tunahitajiana mmoja kwa mwingine, kama kaka na dada; na tukiheshimu hadhi ya utu wa kila mmoja na hivyo kumtukuza Yesu katika wao (cf. Mt 25:40). Yesu alituhakikishia kwamba kwa jinsi tunavyotoa ndivyo tunavyopokea pia (cf. Lk 6:38); Hivyo matendo yetu ya upendo yanakuwa chanzo cha utajiri wa kiroho, kwa kuwa hufungua mioyo yetu na kubadilika na kukutana na Bwana.







All the contents on this site are copyrighted ©.