2014-08-08 16:12:19

Salini kwa ajili ya Iraq!


Wakati huu ambapo hatima ya Wakristo nchini Iraq iko mashakani kutokana na mashambulizi na madhulumu wanayofanyiwa, Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini na watu wpte wenye mapenzi mema kujiunga pamoja naye, ili kusali kwa ajili ya kuwaombea Wakristo nchini Iraq na Jumuiya za Kikristo ambazo kwa sasa zinakabiliana na madhulumu ya kidini!

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake wa pili, Ijumaa tarehe 8 Agosti 2014 kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, anawaalika kwa mara nyingine tena waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kutenga muda kidogo kwa ajili ya kusali kwa watu wote nchini Iraq ambao wanalazimika kuyakimbia makazi yao kutokana na vurugu za kidini.







All the contents on this site are copyrighted ©.