Familia inapaswa kutawaliwa na maneno matatu, samahani, Asante na tafadhali- Papa
Baba Mtakatifu Francisco, amepeleka ujumbe kwa Kongamano la Kimataifa la Amerika ya
Kusini linalojadili masuala ya familia. Kongamano hili limeandaliwa na Baraza linalounganisha
Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Amerika ya Kusini (CELAM), chini ya mada kuu: Familia
na Maendeleo ya Kijamii kwa ajili ya ukamilifu wa Maisha na umoja wa katika utume.
Kongamano hili la siku tano 4-9 Agosti, majadiliano yake yanalenga kutoa mchango katika
Sinodi maalum juu ya Familia, itakayofanyika Vatican mwezi Oktoba 2014.
Ujumbe
wa Baba Mtakatifu unatoa mchango katika swali linalouliza: familia ni nini? Anasema,
licha ya matatizo yake makubwa, na mahitaji yake ya kidharura, familia ni kiini
cha upendo,wenye kutawaliwa na sheria ya kuheshimiana na kushikamana na uwezo wa kuhimili
mashambulizi ya kudanganywa na utawala wa nguvu za dunia. Katika miali upendo wa
nyumbani, mtu huwa na hisia kali za kutambua yeye ni mmoja wa wanafamilia katika asili
yake ya usawa katika kundi binadamu, na hivyo hukabiliana na upinzani potofu wa uongo
kati ya mtu binafsi na jamii.Katika asili yake, ndani ya familia, hakuna hata mmoja
anayetegwa: watoto na mzee hupokelewa na mna utamaduni wa kukutana na kuzungumza kwa
uwazi katika hali za mshikamano na huduma zake kwa makuzi ya watoto.
Na
hivyo Papa anasema, familia ina thamani kubwa, ni hazina na utajiri wa jamii, (kama
alivyoandika Papa Benedikto XVI, katika waraka wake wa Upendo katika Ukweli , 44).
Kwa maana hiyo, alipenda kusisitiza mambo mawili muhimu katika mchango wake, nayo
ni msingi wa : utulivu na uzazi.
Baba Mtakatifu Francisco , kwanza ametaja
misingi ya uaminifu katika ndoa hata mpaka kufa, na ndivyo ilivyo kwa familia hujifunza
maisha ya ndoa, maana ya kuwa mzazi na kuwa ndugu na kuishi ndani ya kaya moja .
Mahusiano haya huunda msingi wa jamii ya binadamu, katika mshikamano, usawa na akili
ya kujisikia kuwa sehemu ya watu, kujisikia karibu, na kujali waliobali mbali zaidi
na au wale ambao kimaisha hawakubahatika. Majiundo haya ya moyo wa ubinadamu katika
mahusiano na wengine, hujenga usalama msingi kwa mtu kuwa tayari kuhudumia wengine .
Baba Mtakatifu anaendelea kueleza kwamba, upendo wa familia ni matunda mazuri
si tu kwa sababu huzaa maisha mapya, lakini pia kwa sababu hukuza upeo wa macho katika
uwepo wake , na ujenzi wa ulimwengu mpya,. Inafaa binadamu kuamini hilo, na kukata
tamaa hila zote za kutaka kushindwa kutimiza misingi ya familia , hasa mshikamano
misingi, heshima na uaminifu. Papa aliendelea kuangalisha katika hatari za kidunia
zinazokabili familia, na hasa kupenda mali za dunia kupindukia, hata kupunguza umuhimu
wa familia katika misingi yake ya kupanuka na kutumikia.
Hatimaye,
Baba Mtakatifu alitoa shukurani zake za dhati kwa uwepo wa uzoefu huu uliosimikwa
katika misingi ya familia , ambamo binadamu hukua katika uwazi wa kumwona Mungu kama
Baba. Kwa hili, waraka wa Aparecida, pia unaonyesha kwamba, familia ni lazima kuchukuliwa
si tu kama chombo cha uinjilishaji, lakini pia kama wakala wa uinjilishaji (432 cf.
nn., 435), ambamo ndani mwake, tunaweza kuitafakari sura ya Mungu ,katika fumbo lake
kamili, kama familia na kwa namna hiyo , tunapata kuona upendo wa kibinadamu kama
ishara ya upendo wa Mungu na uwepo wake (Lumen fidei, 52). Katika familia, imani
na upendo huchanganywa na maziwa ya mama. Papa Francisco ameeleza na kutaja mazoea
ya famlia kuomba kwa hiari baraka kama inavyofanywa na wengi , ni mfano halisi wa
uongofu wa kibiblia kwamba baraka za Mungu, hupitishwa kutoka kwa baba hadi kwa wana.
Kufahamu kwamba upendo familia una thamani kubwa, na kwamba kila tendo la
binadamu linapaswa kuongeza thamani ya familia, na hivyo, ni muhimu kuhamasisha
familia kujenga uhusiano mzuri miongoni mwa wanachama wake, kujua jinsi ya kusema
kwa kila mmoja, bila kupoteza maneno makuu matatu: Nisamehe, Asante, na tafadhali,
na kumgeukia Mungu, Jina nzuri la Baba wa Mbinguni
Papa Francisco amemalizia
ujumbe wake kwa kuomba Msaada wa Mama yetu ya Guadalupe awezeshe kutoa baraka tele
za Mungu kwa ajili ya familia za Marekani na katika kuzaa mbegu za maisha yenye maelewano
na imani thabiti yenye kulishwa kwa Injili na matendo mema. Papa pia amewaomba wasisahau
kuomba kwa ajili yake, maana anahitaji maombezi yao. .