2014-08-06 10:32:55

Vyama vyote Msumbiji, ruksa kushiriki uchaguzi mkuu!


Tume huru ya uchaguzi nchini Msumbiji imetangaza kwamba, hakuna chama chochote cha kisiasa nchini humo ambacho kinazuiliwa kushiriki kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni nchini Msumbiji. Hii ni hatua muhimu sana katika mchakato wa kutaka kulinda, kujenga na kudumisha misingi ya haki, amani na demokrasia ya kweli. Msumbiji inatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba, 2014.

Tangu mwaka 2013 Msumbiji ilijikuta ikiingia tena kwenye kinzani na migogoro ya kijamii iliyopelekea wasi wasi wa kuzuka tena kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe, pale ambapo Chama cha Upinzani cha RENAMO kilipoamua kupimana nguvu na Majeshi ya ulinzi na usalama ya Serikali ya Msumbiji. Katika kujenga mahusiano ya amani na utulivu, RENAMO na FRELIMO wamehitimisha kuratibu mambo msingi yatakayoingizwa kwenye waraka wa utekelezaji wa amani na utulivu nchini Msumbiji.







All the contents on this site are copyrighted ©.