2014-08-04 11:20:34

Waandishi wa habari saidieni mchakato wa Uinjilishaji Mpya!


Shirikisho la Waandishi wa Habari Wakatoliki, UCAP, hivi karibuni limefanya mkutano mkuu na wajumbe kumchagua Bwana George Sunguh kutoka Kenya kuwa ni Rais wa UCAP. Bwana Desire Baiere kutoka DRC amechaguliwa kuwa Makamu wa kwanza wa Rais na Victoria Lugey kutoka Ghana kuwa Makamu wa pili wa Rais. Wajumbe wamemchagua Bwana Rodrigue Dembele kutoka nchini Mali kuwa katibu mkuu wa UCAP na Bwana Eleophas Tyenou kutoka Mali anakuwa mtunza hazina.

Uchaguzi huu umefanyika katika maadhimisho ya mkutano mkuu wa UCAP uliokuwa unafanyika Jimbo kuu la Bamako, nchini Mali. Askofu mkuu Jean Zerbo wa Jimbo kuu la Bamako katika Ibada ya Misa takatifu, amewataka waandishi wa habari kuhakikisha kwamba, wanasaidia utekelezaji wa mchakato wa Uinjilishaji Mpya, kwa kuwapatia watu kweli za Kiinjili, ili kujenga na kuimarisha misingi ya haki, amani, upendo na mshikamano wa kweli.

Anasema mkutano huu umefanyika nchini Mali ambako wakati huu Mali inakabiliana na changamoto mbali mbali zinazotokana na kinzani za kijamii. Mkutano huu umehudhuriwa pia na padre Janvier Yameogo, afisa kutoka Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Jamii pamoja na Bwana Benedict Assorow, Msremaji mkuu wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar, SECAM.







All the contents on this site are copyrighted ©.