Tunasikitika kutangaza kifo cha Kardinali Edward Beda Clancy, Askofu Mkuu Mstaafu
wa Sydney, kilichotokea Jumapili iliyopita, 3 Agosti 2014, kama ilivyotangazwa na
Ofisi ya Mjumbe wa Papa Australia .
Kardinali Edward Beda Clancy, amefariki
akiwa na umri wa miaka 90. Alifanywa kuwa Kardinali na Papa Yohana Paulo II katika
kikao cha Makardinali cha Juni 28, 1988. Alijiuzuru kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu
la Sydney Machi 26, 2001.
Kwa Kifo cha Kardinali Clancy , Dekania ya Makardinali
sasa imebaki na Makardinali 211 Makardinali, ambao 118 ni wapiga kura na 93 si wapiga
kura.
Marehemu Askofu Mkuu Mstaafu Edward Beda Clancy wa Sydney, alizaliwa
Desemba 13, 1923 Lithgow, katika Jimbo la Bathurst. Baada ya kumaliza masomo yake
katika shule katika Richmond na Santa Monica, alijiunga na Chuo cha Mapadre Maria(
Marist) cha Parramatta. Alipadrishwa Julai 23, 1949 na Kardinali Gilroy Na mwaka
1952 alipelekwa Roma kuendelea na masomo katika Chuo cha Mtakatifu Petro , ambako
alifuzu katika teolojia na Maandiko Matakatifu katika Taasisi ya Kipapa ya Biblia
, katika Chuo Kikuu cha Urbaniana. 1955 - alirudi Australia na kuhudumu katika
parokia ya Elizabeth Bay na Liverpool. Nel Februari 1958 aliteuliwa kuwa Profesa
wa Maandiko Matakatifu katika Chuo cha Mtakatifu Columba cha Sprinfield. Na aliteuliwa
kuwa Kasisi katika Chuo Kikuu cha Sydyney na Profesa wa Maandiko Matakatifu katika
Chuo cha Mtakatifu Patrick cha Manly. Oktoba 25, 1973 aliteuliwa kuwa Askofu wa
Jina wa Kanisa la Ardi Carna na baadaye kufanya Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la
Sydney, na kuwekwa wakfu wa Askofu Januari 19, 1974, Katika ibada iliyoongozwa na
Askofu Mkuu wa Sydney, Kardinali Freeman.
Na Novemba 24, 1978 alifanywa kuwa
Askofu Mkuu waJimbo Kuu la Canberra. Mwaka 1983, Papa Yohana Paulo 11 alimteua kuwa
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Sydney. Na 28 Juni 1988,alifanyw akuwa Kardinali . Aliongoza
Jimbo Kuu la Sydney hadi Machi 2001, alipostaafu kwa mujibu wa umri. Pamoja na nyadhifa
nyingine za kitume , kati ya 1986 na 2000, alikuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki
la Australia . Na pia akiwa Mjumbe wa Kamati ya Kimataifa ya Kiingereza katika Liturujia.
Ni aliwahi kuwa Naibu Mwenyekiti wa tisa, wa Mkutano Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu wa
1994, juu ya maisha yaliyowekwa wakfu. Mungu amlaze pema peponi.