2014-08-04 15:30:24

Papa atoa msamaha kwa Padre Brockmann, kuadhimisha tena Fumbo la Ekaristi Takatifu!


Baba Mtakatifu Francisko ametoa msamaha kwa Padre Miguel D'Escoto Brockmann, mwenye umri wa miaka 81kutoka Shirika la Wamissionari wa Maryknoll aliyekuwa amesimamishwa kutoa huduma za Kipadre kutokana na kujihusisha na masuala ya kisiasa.

Adhabu hii ilitolewa kwenye miaka 1980 na wakati wote huu Padre Brockmann amekuwa akitumikia adhabu hii kutokana na kujihusisha kwake na masuala ya kisiasa nchini Nicaragua, ingawa tangu wakati huo aliendelea kubaki mwaminifu kwa Shirika lake la Myarknoll. Kwa miaka kadhaa sasa Padre Brockmann alikuwa maeachana na masuala ya kisiasa. Hivi karibuni ameamua kwa utashi wake mwenyewe kumwandikia barua Baba Mtakatifu Francisko akiomba huruma ili aweze kuadhimisha tena Fumbo la Ekaristi Takatifu kabla ya kuitupa mkono dunia, ombi ambalo limeridhiwa na Baba Mtakatifu Francisko!

Baba Mtakatifu ametoa maagizo kwa mkuu wa Shirika la Wamissionari wa Maryknoll kumsaidia ndugu yake katika Kristo katika mchakato wa kurudi tena katika maisha na utume wa Kanisa kama Padre Mkalatoliki.







All the contents on this site are copyrighted ©.