2014-08-04 11:51:12

Maskauti : Ninyi ni watendaji na si watazamaji tu katika dunia hii.


Salini na kuombea amani barani Ulaya , na wala msiwe na hofu kulinda maadili ya Kikristo. Ni mwaliko Papa kwa Chama cha Maskauti barani, alioutoa katika ujumbe wake, katika matazamio ya kukutana na wawakilishi wa chama hicho wanaendelea na Mkutano wao wa Nne wa kimataifa, hadi Augosti 10, 2014. Mkutano huu unahudhuriwa na wajumbe karibia 12,000 watoto kutoka nchi 20, waliokusanyika huko Normandia, kama sehemu ya kumbukumbu ya kutimia miaka 100, tangu ilipozuka Vita Kuu ya Dunia. Katika ujumbe wake , Papa Francisco anawakumbusha Maskauti wote kwamba, wao ni watendaji katika dunia hii, na si watazamaji. Na anawataka wapeleke Injili ya Upendo wa Kristo ktika mipaka yote ya dunia.

Ujumbe wa Papa umetazamishwa katika hotuba yake aliyoitoa na kuwakabidhi wakati akiwa Rio De Janeiro, Brazil, ambamo aliwaambia, " muhimu kumtambua Yesu na kutembea pamoja naye katika njia ya Maisha , na hivyo wataweza kugundua kwamba, Mungu hutufanya kukutana naye katika njia nyingi: kama vile kupitia uzuri wa viumbe wake, au wakati upendo wake unapoingilia katika historia ya maisha yetu, au katika mahusiano ya kindugu na huduma kwa wengine n.k.

Katika ujumbe huu, Papa Francisco amewataka Maskauti wa Ulaya, kutokuwa na na hofu, kutumikia. Aliwaamba Yesu anawaita wote kwenda, tena kwa nguvu kukutana na Mungu kwa njia ya sakramenti na kuungwa mkono na upendo wake wenye kuondosha hofu zote. Kutangaza upendo wake hadi mwisho wa dunia, kupitia huduma kwa wengine hata katika vitongoji mbali zaidi.

Papa alionyesha kutambua kwamba, vizazi vingi vya Maskauti vimepita, vikitoa mafundisho yanayolenga katika ukuaji wa Maskauti katika utakatifu, mazoezi ya nguvu, na hasa ukuu wa roho. Kwa hili, tukio la kupita kwa miaka mia tangu ilipozuka Vita Kuu ya Kwanza, Papa ametoa mwaliko kwa Maskauti , kuzama katika sala na maombi kwa ajili ya Ulaya umoja na amani, akionyesha matumaini yake kwa Maskauti kwamba wao ni watendaji na si watazamaji tu. Na kisha anawahimiza wasiwe na hofu, iwapo watapambana na vipingamizi na changamoto katika kulinda maadili ya Kikristo, hasa ulinzi wa maisha, maendeleo, hadhi ya binadamu, mapambano dhidi ya umaskini, na mengine mengi yanayo rarua uso wa dunia kila siku. Papa anasema, wakati wote safari huwa ni ngumu, lakini kwa upendo na msaada wa Kanisa, ambao ni Mama wa Wote, wanaitwa kuwa watu wa upendo na kutumikia kwa furaha na ukarimu katika ujana wao.

Ujumbe wa Papa kwa Maskauti, ameeleza Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Maskauti barani Ulaya , Nicoletta Orzes , kwamba unawatia nguvu za kuendelea na njia hii ya Maskauti kama sehemu ya elimu katika mwingiliano wa watu , na kwa mujibu wa ubinadamu wa Ukristo na heshima ya kila mmoja, iwe mwanamke au mwanamme, Mungu ana mpango wake wa Maisha.
Na Padre Bonguslaw Migut, Msaidizi katika Shirikisho la Umoja wa Maskauti Ulaya anasema, Papa anawataka Maskauti, washiriki katika kazi za Kuitangaza Injili ya Kristo, na hasa kupitia shuhuda za maisha.








All the contents on this site are copyrighted ©.