2014-07-28 12:10:28

Papa azungumzia ubunifu, umoja na Askofu na kuwa karibu na watu.


Jumamosi Baba Mtakatifu akitembelea mji wa Caserta , ulio karibu na mji Mkuu wa Naples Kusini mwa Italia, alipata muda wa kukutana na Mapadre wa Caserta kabla ya kuongoza Ibada ya Misa , katika uwanja wa jengo la kifahali la kifalme katika mji wa Caserta.

Mkutano wa Papa na mapadre, katika ukumbi wa Kanisa dogo la Palatine ndani ya jengo la Kifalme la Caserta, ulidumu kwa muda wa saa moja hivi, ulifanyika katika hali ya majadiliano ya kirafiki ya ndani ya familia moja kubwa, wakilishwa na Roho Mtakatifu na mioyo iliyo inuliwa kwa furaha kuu.

Askofu D’Aduse wa Jimbo Katoliki la Caserta , akimkaribisha Papa , alisema kwao, ziara hii imekuwa ni neema kubwa na baraka , na hasa kwa kuwa imekwenda sambamba na Siku Kuu ya Msimamizi wa eneo lao Mtakatifu Anna Mama wa Bikira Maria .

Kama inavyotokea mara nyingi katika mikutano ya namna hi , Papa Francisco aliweka kando hotuba aliyoiandaa na kuanza kujibu maswali ya Mapadre, akisema nilikuwa nimeandaa hotuba lakini sasa sitazungumzia yaliyomo katika hotuba hiyo, badala yake nitaituma kwa Maaskofu. Hivyo Papa aliendesha kipindi cha mwaswali na majibu. Swali la kwanza ikiwa, ni juu ya utambulisho Padre katika kipindi hiki cha Milenia ya Tatu?

Papa alijibu, utambulisho wa kwanza wa Padre kwa wakati hii ni ubunifu katika maisha ya kiroho. Na ubunifu huo hufanikishwa tu ka njia ya maombi na sala. Alisitiza, kuwa mbunifu hakuna njia nyingine,zaidi ya maombi ya kiroho kwa Yesu. Askofu asiye sali au Padre asiye sali huyo ameifunga milango ya roho yake , amefungia njia za ubunifu nje.

Papa aliendelea kuelezea kufafanua kwamba mapinduzi anayozungumzia si mapanduzi katika mambo ya kawaida madogomadogo, lakini ni mapinduzi thabiti katika wogofu, mapinduzi yanayotoka kwa Roho Mtakatifu ambayo mara nyingi huzusha upinzani ndani ya Moyo, kama ilivyokuwa kwa Mtakatifu Rosimini. Kwa mara nyingi mapinduzi ya kweli ya kiroho, huandamana kukubali kuubeba msalaba wa Kristu. Rosimini alikuwa mtu wa sala, na aliandika kwamba, Roho Mtakatifu alimfanya kulisikia hilo na kwa ajili ya hilo alikwenda gerezani kiroho, yaani, nyumbani kwake, hakuweza kusema, hakuweza kufundisha, hakuweza kuandika, vitabu wake ndivyo vikawa kielelezo chake, na leo hii ni Mtakatifu. Kwa mara nyingi ubunifu katika maisha ya kiroho, huongoza katika msalaba.


Maombi hufungua Mlango kwa Mungu na jirani, nandivyo kanisa linavyotakiwa daima kuwa wazi na si kujifungia lenyewe, bali ni lazima liwe karibu na watu wengine bila ubaguzi wowote wala hofu yoyote. Mtu wa Mungu daima haongopi lolote bali huwa na ujasiri wa kujongea karibu na kila mmoja, hasa kupitia njia ya mazungumzano. Mazungumzano ni muhimu. Lakini kwa Padre au muumini yoyote , kabla hajaingia katikamajadiliano na wengine ni lazima kwanza , aufahamu utambulisho wake mwenyewe, kama kianzio , pili ni muhimu kujitahidi kuwaelewa wengine.


Papa alionya kwamba , iwapo mtu hana uhakika na utambulisho wake, itakuwa vigumu kujiwasilisha na kushiriki katika majadiliano na wengine. Alisema huwezi kuizungumzia imani yako iwepo wewe mwenyewe, hujajilisha sawasawa ufahamu wa imani yako, kama mwanzo wa utambulisho wako wenyewe. Kama wewe mwenyewe hujielewi sawasawa , utawezeje kukosoa wengine? Papa alihoji na kuongoza yafaa kutambua kwamba, kila mtu, kila mwanamke ana kitu cha kutoa kwa mwingine , na kila binadamu ana historia yake mwenyewe, hali yake wenyewe na Mapadre wanapaswa kuwa wau wa kuskiliza kwanza, kisha katika utulivu na busara ya Roho Mtakatifu, wataweza kutoa jibu kwa maswali yanayoulizwa. Kwa mtu wa imani , jibu daima hutoka kwa Roho Mtakatifu.

Papa aliendelea kuwaambia Mapadre , hakuna sababu ya kumwongopa binadamu mwingine,bali waendelee kutembea katika nji aya majadiliano na wengine si kwa lengo la kutaka kuongoa mwingine kwa lazima, lakini majadiliano yanayo lenga kuleta uelewa zaidi a mmoja kwa mwingine. Na ndivyo Kanisa linapanuka si kwa kulazimisha uongofu kwa wengine lakini kwa kulifahamu, huvutia wengine kujiunga nalo.








All the contents on this site are copyrighted ©.