Tanzia:Kardinali Francisko Marchisano amefariki dunia.
Tunasikitika kutangaza kifo cha Muadhama Kardinali Francisco Marchisano , Padre Mkuu
Mstaafu wa Kanisa Kuu la Kipapa la Mtakatifu Petro la Vatican, kilichotokea leo Jumapili
27 Julai majira ya sa nne nyumbani kwake. Kardinali amefariki akiwa na umri wa miaka
85.
Aliteuliwa kuwa Kardinali Octoba 21 2003. Na alifanya utume mbalimbali
katika Ofisi za Curia ya Roma , ikwemo kuwa Rais wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya mapokeo
ya utamaduni wa Kanisa na pia akiwa Rais wa Tume ya Mambo ya Kale Matakatifu. Na alifanya
kuwa Msimamizi Mkuu wa utawala wa jiji la Vatican , Licha ya kuwa Rais wa Taasisi
ya Mtaktifu Petro na Rais wa Ofisi kuu ya kazi ktiak Jimbo Takatifu.
Aidha
taarifa inabaini kwamba, maziko yataongozwa na Mkuu wa Dekania ya Makardinali , siku
ya Jumatano 30 Julai katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro hapa Vatican . Papa Francisco
atahudhuria Ibada hii na atatoa neno la mwisho na baraka.
Kwa kifo cha Kardinali
Marchisano, Decania ya Makardinali kwa sasa imebaki na Makardinali 212, ambao kati
yao 118 wana haki ya kupiga kura na 94 hawana haki ya kupiga kura ya kumchagua Papa
kwa mujibu wa sheria ya conlave.