2014-07-27 15:15:07

Jibu la kuzima maovu yote ni kusema hapana kwa kila ovu na uvunjaji wa sheria-Papa


Jumamosi 26 Julai, majira ya alasiri, Baba Mtakatifu alifanya ziara ya Kichungaji katika mji wa Caserta ambako alikutana na viongozi wa Kanisa Katoliki na Kiinjili, na kuongoza Ibada ya Misa katika uwanja wa mji huo.

Papa alikwenda Caserta kwa kutumia usafiri wa helkoputa , na mara baada ya kuwasili alipokelewa na uongozi wa Caserta, Askofu Giovanni D’Alise , wa Jimbo Katoliki la Caserta, Dr Carmela Pagano , Msimamizi Mkuu wa utawala wa Caserta, Bwana Pio Del Gaudio , Meya wa Caserta , Rais wa Mkoa wa Caserta Domenico Zinzi na pia Kamanda Mkuu wa kikosi cha Kijeshi katika eneo hilo, Kanali Vieniero Santori, kwa utaja wachache.
Baada ya Mapokezi, alIsalimiana na Mapadre na wenyeji wa Caserta na baadaye kuongoza Ibada ya Misa Takatifu katika uwanja wa Reggia di Caserta, ulio mbele ya jengo la Kifalme la Caserta ambalo yalikuwa ni makazi ya Mfalme wa Naples nyakati za kale.

Homilia ya Papa katika Ibada hiyo ilisisitiza, semeni hapana kwa kila ubaya na uvunjaji wa sheria. Na kwamba, uongofu wa moyo unadai kuwa watu wema, kumpokea kwa moyo mkunjufu kila mhitaji.

Papa alisema, kurithi Ufalme wa Mungu, Wakristo wanapaswa kumweka Mungu kwanza katika maisha yao. Na alisisitiza uwepo wa Yesu ndani ya mioyo yetu, hubadili maisha yetu, na kutufanya tujali pia mahitaji ya ndugu zetu. Maisha maongofu hivyo yanakuwa ni wito unaoalika kila mmoja kumkubali mwingine hasa mtu mhitaji , wakiwemo wakimbizi, wageni na wahamiaji.

Na kwamba kumpa Mungu nafasi ya kwanza kuna maana ya kuwa na ujasiri wa kusema hapana, kwa mabaya, vurugu, ukandamizaji; ni kuishi maisha ya huduma kwa wengine nyenye kujali sheria kikamilifu kwa ajili ya manufaa ya wote.

Katika homilia hiyo , Papa aliendelea kusema, wakati mtu anapopata kuwa na hazina ya kweli kutoka kwa Mungu, huachana na ubinafsi na hutafuta kila namna ya kuwashirikisha wengine upendo wa Mungu. Kwa kuwa yeye aliye rafiki wa Mungu, huwapenda ndugu zake, na pia huheshimu na kulinda maisha na ustawi wao, na pia huheshimu mazingira na asili, Papa Francisco , alieleza kwa kurejea muhimu wa kutunza mazingira kama ulivyo uzuri wa eneo la Campania, ambalo alisema linahitaji kulindwa na kutunzwa kama lilivyo.

Ili kufanikisha hilo, Papa alisisitiza kunahitaji kila mtu kuwa na moyo wa kupenda kutumikia kweli, na kuishi maisha maongofu ya Kiinjili , ambayo ni wazi kama zawadi ya binafsi na makini kwa watu wengine hasa maskini na waliotengwa kutokana na hali zao.

Katika homilia yake , Baba Mtakatifu alilenga zaidi katika kutafakari nini maana ya Ufalme wa Mungu, akirejea maneno ya Yesu ambayo yalizungumza katika lugha nyepesi ya kueleweka kwa watu , kwa mfano mfupi ulioandikwa katika injili,wahazina iliyofichika katika shamba na Mkulima maskini na mfanyabiashara tajiri aliyekuw aakisafiri huko na kule kutafuta mali.
Papa aliendelea kufafanua, Mfanyabiashara maisha yake yote aliyaelekeza katika kutafuta kitu cha thamani, ambacho kitaweza kuzimisha kiu yake kwa uzuri na hivyo kusafiri duniani kote, bila ya kujihurumia, akilishwa na tumaini la kupata kila alichokua akikitafuta. Na upande mwingine, mkulima, ambaye hakuwa na wazo la kwenda mbali ya shamba lake , muda wote alifikiri tu kufanya kazi kwa bidii ili ajipatie riziki yake ya kila siku. Lakini hatima yake anagundua utajairi huu mkubwa , hazina ya thamani , lulu moja ya thamani kubwa.

Na hivyo nini maana ya mfano huu ? Papa Francisiko alisema, Yesu anazungumzia furaha ya kuingudua hazina ya thamani katika maisha hata hapo ulipo, hata bila ya kusafiri au kutangatanga huko na kule. Ni kusikiliza Neno la Injili na kuliishi, tunapata a lulu ya thamani ya ufalme wa Mungu hapa duniani. Kwa maneno mengine ni kuwa mema; na kumweka Mungu kwanza katika maisha yetu, na kuwapenda wengine kwanza.

Maisha boya kwa Mungu, maana yake kuwa na ujasiri wa kusema hapana kwa mabaya, vurugu, uonevu, na kuishi maisha ya huduma kwa wengine na kwa ajili ya sheria na manufaa ya umma. Maisha bora ni kumwona Mungu kuwa ndiye hazina ya kweli, ni kuondokana na maisha ubinafsi na kujaribu kushirikiana na wengine upendo unaotoka kwa Mungu ambaye ni rafiki na kila mmoja. Ni kuyalinda maisha, na kuheshimu mazingira na asili. Maisha maongofu ni kuwa na ujasiri wa kusema hapana kwa nia yoyote ya rushwa na uvunjaji wa sheria. Iinahitaji kila mtu kuwa mhudumu wa ukweli na kuchukua katika kila mfumo wa maisha ya kiinjili ambayo ni uwazi katika zawadi maisha binafsi, na kuwapenda wengine- hasa maskini.

Jumamosi pia Papa aliongoza Ibada hiyo katika eneo la Caserta kwa heshima ya Mtakatifu Anna, Mama wa Yesu, ambaye pia ni mlinzi wa mji wa Caserta. Kwa ajili ya Siku Kuu hiyo, Papa aliwahimiza wakazi wote wa mji wa Caserta, wakiwa wamewazunguka viongozi wao wa Kikanisa na Kiserikali pia , kuiishi sikukuu ya mlinzi wao, kwa kwa kutakatifusha imani yao na kuitambua familia ya Mungu kuwa kifungo cha nguvu katika kujenga udugu na mshikamano kati yao. Kuwa na ujasiri kama ilivyokuwa kwa binti yake Maria baada ya kupaswa habari alisema Mungu amefanya Mambo makuu kwa mkono wake: "amewashusha wenye nguvu kutoka vitI vyao vya enzi, na kuwakweza wanyenyekevu, wenye njaa amewashibisha na matajiri amewaondoa mikono mitupu Lk 1, 51-53). Na hiyo ni kumtumainia Bwana tunapoitatufa hazina ya kipwkee iliyofichika , hazina pekee ni Yesu mwenyewe, anayefundisha mbinu za kugundua vigezo vya Mungu







All the contents on this site are copyrighted ©.