2014-07-25 15:36:51

Papa apanga mstari na kupata chakula cha mchana na wafanyakazi wa Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 25 Julai 2014 amekwenda kutembelea Bwalo la chakula kwa ajili ya wafanyakazi wa Vatican na kushiriki pamoja nao chakula cha mchana! Baba Mtakatifu amejipanga mstari kama wafanyakazi wengine na kuhudumiwa kama wafanyakazi wengine.

Baba Mtakatifu wakati wa chakula cha mchana amezungukwa na Familia yake kubwa, watu wa nyumbani kwake, wanaomsaidia katika utekelezaji wa dhamana yake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Amezungumza na wapishi pamoja na wahudumu na amefurahishwa na mapishi yao, kiasi kwamba, wengi wa wapishi wamebaki wakiwa wameshika tama! Baba Mtakatifu amekaa bwaloni hapo kwa muda wa saa nzima hivi. Kwa hakika wanasema wafanyakazi wanaohudumia Bwaloni hapo kwamba, wamefurahi kupita kiasi!







All the contents on this site are copyrighted ©.