2014-07-25 15:59:52

Papa aguswa na msiba wa ajali ya ndege, Algerie!


Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa kwa taarifa ya ajali ya ndege iliyotokea Alhamisi, tarehe 24 Julai 2014, Kaskazini mwa nchi ya Mali, ikiwa na abiria 118 na kuanguka baada ya kuwa imekwisharuka kwa takribani dakika 50. Abiria wote waliokuwa kwenye ndege hii kutoka nchini Hispania kwenye Kampuni ya Swiftair na kukodiwa na Shirika la ndege la Algeria, Air Algerie. Ndege hii ilikuwa inasafiri kutoka Ouagadougou, Burkina Faso kuelekea Algeri, nchini Algeria.

Katika ujumbe uliondikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwenda kwa Askofu mkuu Ghaleb Bader wa Jimbo kuu la Algeria, Baba Mtakatifu anaungana na watu wote waliofikwa na msiba huu mzito na anawaombea kwa Mwenyezi Mungu, ili aweze kuwapatia raha ya milele marehemi wote waliopoteza maisha yao kwenye ajali hii. Anawaombea faraja wote walioguswa na msiba huu!







All the contents on this site are copyrighted ©.