2014-07-25 12:37:06

Majembe mapya ya AMECEA!


Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati, AMECEA baada ya kumchagua Askofu mkuu Berhaneyesus D. Souraphiel kuwa Mwenyekiti mpya wa AMECEA, wameridhia kwamba, Padre Ferdinand Lugonzo kutoka Jimbo Katoliki la Kakamega ataendelea kuwa Katibu mkuu wa AMECEA kwa awamu ya pili. Monsinyo Pius Rutechura kutoka Jimbo Katoliki la Bukoba ataendelea kuwa Makamu wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki na Kati, CUEA.

AMECEA imewateuwa Kardinali Polycarp Pengo, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Tanzania, Kardinali John Njue, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Nairobi, Kenya, Askofu mkuu Tarcisio Ziyaye wa Jimbo kuu la Lilongwe, Malawi pamoja na Askofu Anthony Muheria kutoka Kenya kuwa ni Wajumbe wa Bodi ya Udhamini ya AMECEA.

AMECEA imewateua Maaskofu wafuatao kuwa kwenye Bodi ya Watendaji wakuu wa AMECEA nao ni: Askofu Tesfaselessie Medhin kutoka Ethiopia; Askofu Michael Didi kutoka Sudan, Askofu Thomas Msusa kutoka Malawi, Askofu Athony Zziwa kutoka Uganda, Askofu Philip Anyolo, kutoka Kenya, Askofu Charles Kasonde kutoka Zambia na Askofu Rogatus Kimario kutoka Tanzania kuwa wawakilishi wa Bodi ya watendaji wakuu wa AMECEA.

Askofu Maurice Muhalia Makumba kutoka Kenya amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha CUEA. Wajumbe wengine ni pamoja na: Askofu Sabino Odoki kutoka Uganda; Askofu Abraham Desta kutoka Ethiopia, Askofu Martin Mtumbuka kutoka Malawi, Askofu Alick Banda kutoka Zambia pamoja na Askofu Bernadin Francis Mfumbusa kutoka Tanzania.







All the contents on this site are copyrighted ©.