2014-07-24 15:48:32

Mchezo Kimataifa wa soka kwa ajili ya amani


Taarifa imetolewa kwamba, hapo tarehe Mosi Septemba 2014 , katika uwanja wa Michezo wa "Olimpic" wa jijini Roma, kutafanyika shindano la mpira wa miguu, ambao wachezaji wake watatoka madhehebu mbalimbali ya kidini, kwa lengo la kuhamasisha amani duniani.

Tukio hili la kimataifa linaandaliwa na mashirika ya kujitegemea, "Scholas Occurrentes" na P.U.P.I Onlus". Kati ya wachezaji ni watu walio maarufu katika mchezo wa soka kama kama vile Lionel Messi, Gianluigi Buffon, Zinedine Zidane, Javier Zanetti, Roberto Baggio, Andrea Pirlo, Yuto Nagatomo na Samuel Eto'o. Baadhi wakihojiwa na vyombio vya habari wameeleza kwamba, kila mmoja atashiriki katika mchezo huo, akiwakilisha dhehebu lake" tunaingia sote uwanjani kuwakilisha dini zetu katika uwanja wa amani". Kuonyesha kwamba inawezekana kuishi na kutenda kwa mshikamano na umoja licha ya kutofautiana kiimani.

Juhudi hizi zilianza Aprili, 2013, wakati Papa Francisco, alipokutana na timu ya Italia na timu ya Argentina, baada ya kuwa na mchezo wa kirafiki . Katika tukio hilo, Papa alitoa wazo kwa mmoja wa wachezaji wa soka Javier Zanetti , kuona uwezekano wa kuandaa mchezo unaoweza kushirikisha wachezaji waamini wa dini mbalimbali, kama ishara ya ujenzi na mwendelezo wa udugu na ushirikiano kwa njia ya michezo. Michezo imekuwa ni kati ya matukio yenye kuwaunganisha watu pamoja licha ya tofauti zao za kidini au kitamaduni.

Tiketi za kuingia uwanjani kwa ajili ya tukio hili, zitaanza kuuzwa tangu Ijumaa Julai 25 2014, na fedha zitakazo kusanywa zitatumika katika matendo ya hisani.

"Scholas Occurrentes", ambayo makao yake makuu yako katika Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya Sayansi, ni taasisi za elimu ya umma, iliyoanzishwa na Papa Francisco, kwa lengo la kukuza matumizi ya teknolojia, sanaa na michezo, katika juhudi za ushirikishwaji wa jamii na utamaduni. Na P.U.P.I. Foundation ni Asasi isiyo ya kiserikali, iliyoanzishwa miaka kumi iliyopita na Paula na Javier Zanetti,kwa ajili ya kukuza na kusaidia mipango ya kupanda watoto kwa mbali na pia kwa ajili ya kutoa msaada vijijini na , kupunguza hali mbalimbali ya ugumu wa maisha.








All the contents on this site are copyrighted ©.