Shirika la Misaada Katoliki (CRS) limeahidi kuendeleza msaada wake kwa AMECEA, kwa
ajili ya kufanikisha utekelezaji wa mkakati iliyokubalika kutoa jibu, kwa Waraka
wa Kitume uliotolewa na Papa Benedikto XVI, baada ya sinodi Maalum ya Maaskofu kanda
ya Bara la Afrika, Waraka wenye jina "Dhamana ya Afrika “ (Africae Munus)”.
Akizungumza
katika kikao cha 18 cha AMECEA, Jumamosi iliyopita, Julai 19, 2014, Rais na Afisa
Mtendaji Mtendaji Mkuu wa Ofisi (CEO) ya CRS, Dk Carolyn Woo aliirejea mandhari
iliyofungua Mkutano huo, "Uinjilishaji Mpya, kupitia njia ya Wogofu na kushuhudia
Imani ya Kikristo, kwamba, ni mada makini kwa CRS. "Kutoa ushuhuda wa imani yetu,
hasa miongoni mwa watu wenye shida na waliotengwa na jamii , ni kiini cha utendaji
wote wa shirika hilo la CRS, na mkakati wa shirika katika kuimarisha ushirikiano
wake na wanachama AMECEA, katika mshikamano wa kutoa huduma kwa maskini na wanaoishi
katika mazingira magumu". Dk Woo alieleza jinsi wafanyakazi wa CRS, walivyo tayari
kushirikiana na AMECEA kutathmini yale yaliyokwisha fanikishwa na kile ambacho bado
kinahitaji msukumo nangvu zaidi, tangu kutolewa kwa AfricaeMunus, na katika mtazamo
mpya wa Mipango Mbinu, katika mkakati wa maendeleo ya AMECEA. Na hivyo CRS, inatarajia
kujifunza zaidi juu ya mpango mpya wa miaka 10, kiufundi, vifaa na msaada wa fedha
unaohitaji sasa, ikilinganishwa na siku za nyuma.
Rais alisema, CRS inatambua
changamoto zinazopambanisha watu katika mkoa AMECEA, ikiwemo migogoro ya ndani na
baina ya mataifa, pia yenye kuvuka mipaka ya kidini, hali ya hewa, uhaba wa chakula,
ajira kwa vijana, na biashara ya binadamu nk
Padre Chrsisantus Ndaga, Katibu
wa Kitengo cha Mawasiliano cha AMECEA, anaripoti zaidi kwamba, Rais wa CRS, imeonya
wanachama wa AMECEA kwamba, iwapo matatizo hayo yatabaki bila kupatiwa ufumbuzi, vitisho
hivi vinaweza kwa haraka kubadili mafanikio yaliyopatikana hadi sasa. Na kwa bahati
CRS, imekuwa ikisaidia utekelezaji wa miradi mingi katika ngazi za kijimbo katika
kanda AMECEA. Na kwamba CRS, itaendelea na ushirikiano na kusindikizana katika roho
ya Papa Benedict XVI, aliyoionyesha katika barua yake binafsi, juu ya Fadhila, na
Azimio la 2012 la Kinshasa la Maaskofu wa Afrika.