Vatican Radio) Jumapili Papa Francis alionyesha kuhofia hatma ya jamii ya Kikristo
katika mji wa Mosul Iraq ,na katika sehemu nyingine za Mashariki ya Kati, ambako
kwa wakati huu kuna mapambano makali ya vita vya wenyewwe kwa wenyewe.
Akizungumza
baada ya sala ya Malaika wa Bwana katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,
Papa aliyaelekeza mawazo yake, kwa Wakristo wanaoteseka katika nchi yao, ambayo
wamekuwa wakiishi tangu mwanzo wa Ukristo, akisema ni sadaka yenye mchango thamani
sana kwa manufaa ya jamii zima ya biandamu.
Wakristo hao, ndugu zetu wanateswa!
Hao wametengwa na nyumba zao na kulazimishwa kukimbia bila hata kuwa na uwezo wa kuchukua
mali zao, alieleza kwa masikitiko na kuwahakikishia ukaribu wake na sala za mara
kwa mara. Pia alionyesha kutambua mateso ya wake kwa waume, akisema anafahamu kwa
jinsi gani wanateseka , na kwamba kiimani anateseka pamoja nao hadi hapo katika Jina
la Bwana, uovu utakaposhindwa.
Kisha Papa alitoa wito kwa wote, tangu
wale waliokuwa wakimsikiliza katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro hadi kona
zote za dunia, wadumu katika kuomba kwa ajili ya amani katika hali zote za mivutano
na migogoro duniani , na hasa Mashariki ya Kati na Ukraina. “Mungu wa amani, na
aamushe hamu halisi kwa ajili ya mazungumzo na maridhiano. Kame vurugu haiwezi kuondoa
vurugu. Vurugu ni kujitenga mbali na amani”!
Papa alitoa wito huu, baada ya
kutafakari somo la Injili la Jumapili , ikifuatia na sala ya Malaika wa Bwana. Kwa
ajili ya tafakari kwa somo la Injili ya siku, Papa alieleza maana ya mfano wa mpanzi
uliotajwa katika Injili, mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake na adui yake
usiku kumpandia magugu. Na wakati watumishi wa shamba walipotaka kuyatoa magugu
mapema, bwana wao aliwakataza akisema, watang’oa pia mizizi ya ngano na hivyo ni
vyema kuacha vyote kukua pamoja, ngano na magugu.
Mfano huu - Papa Francisco
alielezea – unazungumzia wakati wetu huu, ambamo watu wema wanaishi na matatizo
ya maovu duniani na inaonyesha uvumilivu wa Mungu.
Shetani , anapanda mbegu
ya maovu ambako kuna mbegu nzuri ya wema, anajaribu kuwagwwa watu , familia na mataifa.
Lakini Mungu anajua jinsi ya kusubiri. Mungu anatazama katika 'shamba' la kila mtu
kwa uvumilivu na huruma: anaona uchafu na uovu vizuri zaidi kuliko sisi, lakini
yeye pia anaona mbegu za nzuri na kwa uvumilivu anasubiri ziote na kukomaa.
Mungu
- Papa Francis alisema - ni Baba Mvumilivu mwenye kusubiri kwa moyo wazi wa kuwakaribisha
wenye kumkosea na husamehe makosa yetu bila kuchoka. Lakini uvumilivu wake hauna
maana kwamba hakichukizwi na maovu. Yeye daima hachanganyi mema na mabaya. Na mwisho,
wakati wa mavuno, Yesu atatoa hukumu kwa wote, kuwatenganisha wale ambao ni mbegu
nzuri kutoka kwa wale ambao ni mbegu ya magugu. Na hivyo Papa ameonya, tutahukumiwa
kwa kipimo hichohicho tunachotumia kuwahukumu wengine, na ni huruma hiyohiyo tutakayopewa
ambayo sisi pia tunaionyesha kwa wengine. Papa alimalizia kwa kuomba msaada wa
Mama yetu Maria , atusaidie kukua katika uvumilivu na katika huruma.