2014-07-18 15:35:36

Papa asikitishwa na ajali ya ndege ya Malaysia!


Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa sana na taarifa kuhusu kutunguliwa kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia, Alhamisi tarehe 17 Julai, katika eneo la Ukraine ambayo kwa sasa imegeuka kuwa ni uwanja wa vita na kinzani. Baba Mtakatifu anawakumbuka na kuwaombea abiria 298 waliofariki dunia katika ajali hii pamoja na wote walioguswa na msiba huu mkubwa.

Baba Mtakatifu anawasihi wahusika wa mgogoro wa vita nchini Ukraine kusitisha vita na kuanza kujielekeza zaidi katika njia za majadiliano, ili kujenga na kudumisha misingi ya haki na amani sanjari na kuokoa maisha ya watu wasiokuwa na hatia yanayoendelea kupotea kutokana na vita!







All the contents on this site are copyrighted ©.