2014-07-17 15:30:02

Papa kutembelea mjini Caserta, hapo tarehe 26 Julai 2014


Katika maadhimisho ya kumbu kumbu ya watakatifu Joakim na Anna, wazazi wake Bikira Maria, inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 26 Julai, Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kutembelea mji wa Caserta, ulioko mkoani Campania.

Saa 12:00 Jioni, Baba Mtakatifu anatarajiwa kukutana na Makleri na hatimaye, kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya waamini wa Caserta kwani Mtakatifu Anna ni msimamizi wa mji huu.

Ufafanuzi huu umetolewa na Padre Federico Lombardi, msemaji mkuu wa Vatican na kwamba, Baba Mtakatifu Francisko atarejea tena mjini hapo Jumatatu tarehe 28 Julai 2014 ili kumtembelea rafiki yake Giovanni Traettino, mchungaji wa Kanisa la Kiinjilisti.







All the contents on this site are copyrighted ©.